title : WAHITIMU 753 CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA KAMPALA TANZANIA WATUNUKIWA VYETI.
kiungo : WAHITIMU 753 CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA KAMPALA TANZANIA WATUNUKIWA VYETI.
WAHITIMU 753 CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA KAMPALA TANZANIA WATUNUKIWA VYETI.
Uongozi wa mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Kampala-Tanzania wakiwa katika mahafali ya kwanza wa chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa Kampala -Tanzania wakitunukiwa vyeti leo jijini Dar es Salaam.
Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Zaidi ya Wahitimu 753 wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala-Tanzania wametunuku vyeti vya astashahada, stashahada, shahada, shahada ya Umahiri baada ya kufanya vizuri katika masomo katika taaluma mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.
Wahitimu hao wamesoma fani mbalimbali kutoka kitivo cha Masomo ya Ualimu na sheria, Kitivo cha Kompyuta, Menejiment na Sayansi za Jamiii, Kitivo cha Sayansi ya Tiba na Famasia.
Akizungumza katika hafla ya Mahafali ya kwanza Chuo cha Kimataifa cha Kampala-Tanzania leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Jamidu Katima, amesema kuwa matumaini ya chuo kufanya vizuri na chachu ya kufanikisha maendeleo taifa.
Profesa Katima amesema kuwa kutokana na elimu waliyopata kwa muda wote walipokuwa chuoni watakwenda kuifanyika kazi katika shughuli mbalimbali.
"Kuna wahitimu tumeishi nao kwa muda wa miaka 3,4 hadi 5 na wengine zaidi ya hapo kutokana na sababu mbalimbali, nawapongeza sana" amesema Profesa Katima.
Katika hatua nyengine Profesa Katima ameeleza kuwa chuo kimeendelea kufanya mabadiliko ili kuhakikisha kinapiga hatua na kuwa chachu ya maendeleo ya elimu hapa nchini.
Amesema kuwa miongoni mwa mabadiliko hayo ni kuunda baraza la Chuo linaloongozwa na Mhandisi Profesa Tolly Mbwete ambaye aliwahi kuwa makamu mkuu wa chuo Kikuu Huria Tanzania pamoja na kuajiri wanataaluma na waendeshaji wenye sifa stahiki kwa mujibu wa miongozo ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
"Tumefanya maboresho makubwa katika muundo wa vitivo, kurugenzi idara mbalimbali ikiwemo kuajiri wakuu wa vitivo ili kuboresha utendaji wetu" amesema Profesa Katima.
Amesema kuwa chuo kinaendelea kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na TCU katika tunatoa elimu bora kwa wanafunzi.
Profesa Katima amesema kuwa changamoto walizopitia katika chuo hicho zimewajenga na kuwaimarisha kimuundo na kitaasisi.
"Kwa sasa chuo kina jumla ya wafanyakazi 269, I38 wanataaluma ambao wanajumuisha maprofesa II na wenye digrii ya uzamivu 20 pamoja na na waendeshaji ni I3I" amesema Profesa Katima.
Hata hivyo ameeleza kuwa miundombinu ya chuo ipo katika mazingira mazuri ambayo ni rafiki kwa wanafunzi.
Mjumbe wa bodi taasis ya Mwalimu Nyerere Kate Kamba, amesema kuwa matumaini yake wahitimu wamepata maarifa na ujuzi katika fani walizosoma.
Kamba alikuwa anamwakilisha mgeni rasmi Rais Mstaafu Dkt. Ali Hassani Mwinyi katika mahafali hayo, amesema kuwa wahitimu wanategemewa kuwa na upeo mkubwa katika kupambana na changamoto watakazokumbana nazo.
"Pamoja na kujiendeleza katika masomo ya juu naomba muwe na utii na uaminifu kazini, mnihakikishie mtakuwa waaminifu na waadilifu na kwamba hamtashiriki kabisa katika ufisadi" amesema Kamba.
Hata hivyo ameutaka uongozi, Baraza na Bodi ya Wadhamini wa Chuo kutatua mapungufu yote pamoja na kuendelea kuwa na ajenda moja ya kufundisha na kufanya utafiti ili kuchangia katika maendeleo ya nchi.
Mwenyekiti wa baraza la Chuo cha Kimataifa cha Kampala- Tanzania Profesa Tolly Mbwete, amewapongeza wahitimu wote kwa kufanya vizuri katika masomo yao pamoja maprofesa na wahadhiri, wafanyakazi kwa kutoa mchango wao wa kupatikana wahitimu.
Amesema kuwa elimu ni nyenzo muhimu ambayo inamuwezesha mtu kukabiliana na changamoto zinazomzunguka, huku akiwataka wahitimu kwenda kuitumia elimu yao katika kuiletea jamii maendeleo.
Hata hivyo Profesa Mbwete, amesema kuwa baraza litahakikisha linasimama imara na kuwa kiunganishi muhimu kati ya elimu na ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Profesa Mbwete amesema kuwa tayari baraza limekwisha anza kazi kwa kufanya vikao viwili na kufanya maamuzi muhimu kwa ajili ya kuimarisha pamoja na kuongeza ufanisi wa shughuli za chuo.
Amesema dira ya serikali ya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sekta ya viwanda, lakini ni vigumu kufika malengo hayo bila kuwa na vyuo vinavyotoa elimu bora.
"Ili kufika malengo tayari baraza kwa kushirikiana na uongozi wa chuo linaendelea kufanya mapitio ya program zake ili kuzalisha wataalamu watakaokabiliana na changamoto" amesema Profesa Mbwete.
Profesa Mbwete ameeleza kuwa tayari baraza limepunguza idadi ya vitivo kutoka saba hadi kufika nne pamoja na idadi ya idara za kitaaluma na kitawala kutoka 2I hadi I0.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Alhaji Hassan, amesema kuwa bodi ya wadhamini inaendelea na mikakati ya kuwekeza katika chuo ili kiendelee kufanya vizuri.
Amesema kuwa kipaombele kwa sasa katika kufanya uwekezaji ni kumalizia ujenzi wa hospitali katika chuo hicho jambo ambalo litasaidia kutoa huduma za afya kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya chuo.
Hata hivyo ameeleza kuwa furaha ya bodi ni kutengeneza fursa za ajira kwa vijana kwa kujiajiri au kuajiriwa kupitia elimu wanayoipata na kusaidia kukidhi mahitaji yao na jamii kwa jumla.
"Wahitimu wote kazi kubwa umeifanya, bodi ya wadhamini inawapongeza, wahadhiri na wafanyakazi wa KIUT kwa kuwafikisha wahitimu hawa katika hatua hii" amesema.
Hivyo makala WAHITIMU 753 CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA KAMPALA TANZANIA WATUNUKIWA VYETI.
yaani makala yote WAHITIMU 753 CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA KAMPALA TANZANIA WATUNUKIWA VYETI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAHITIMU 753 CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA KAMPALA TANZANIA WATUNUKIWA VYETI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wahitimu-753-chuo-kikuu-cha-kimataifa.html
0 Response to "WAHITIMU 753 CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA KAMPALA TANZANIA WATUNUKIWA VYETI."
Post a Comment