Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy

Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy
kiungo : Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy

soma pia


Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy

Na Grace Michael, Nachingwea

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa mpango wa Ushirika Afya ndio njia pekee na ya kisasa inayomwezesha mkulima kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote na kuepukana na upotevu wa fedha nyingi kwa kulipia gharama za matibabu.

Amesema kuwa ili mkulima aweze kunufaika na fedha anazozipata kutokana na kuuza mazao yake ya biashara ni lazima awe na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Ameyasema hayo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma pamoja na uhamasishaji wa wananchi na wakulima kujiunga na mpango wa Ushirika Afya ili waweze kunufaika na huduma za matibabu kwa gharama nafuu.

“Ndugu zangu wana Nachingwea, nafahamu kabisa mmeweka mipango mingi kwenye fedha zenu mtakazopata kutoka kwenye mazao mliyouza lakini niwaombe sana katika vipaumbele vyenu suala la Ushirika Afya liwe ni miongoni mwake, kuwa ndani ya mpango huu kunakusaidia wewe na familia yako kutokupoteza fedha zako unapopatwa na magonjwa,” alisema Mhe. Ummy.

Alifafanua kuwa gharama atakayotumia mkulima huyo kujiunga na Ushirika Afya ni ndogo sana ikilinganishwa na kugharamia huduma za matibabu kwa fedha taslimu hali ambayo imesababisha wananchi wengi kuingia kwenye umasikini kwa kuuza mali zao ili wapate fedha za kujitibia. 

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi fomu 1,000 kwa Kiongozi wa Vyama Vya Ushirika wilaya ya Nachingwea.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikabidhi kadi kwa Mwanaushirika aliyejiunga na mpango wa Ushirika Afya.
 Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi. Rukia Muwango akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Benard Konga wakifuatilia maelezo ya Mhe. Waziri.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mhe. Hassan Masala.
 Wananchi wilayani Nachingwea wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akielezea upatikanaji wa huduma za matibabu.



Hivyo makala Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy

yaani makala yote Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/ushirika-afya-ni-mkombozi-wa-afya-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ushirika Afya ni Mkombozi wa Afya ya Mkulima- Waziri Ummy"

Post a Comment