UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU

UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU
kiungo : UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU

soma pia


UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
CHUO Kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki cha jijini Dar es Salaam, kipo mbioni kujenga kampasi mpya katika eneo la Boko, mradi ambao utaanza mapema mwakani baada ya kukamilika kwa hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka katika taasisi ya Norweigian Gurantee Export Credits (GIEK.)

Akizungumza wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbalimbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi ,2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa  Charles Mgone amesema kuwa ujenzi wa Kampasi hiyo mpya utaongeza idadi ya wadahiliwa pamoja na kuongeza idadi ya kozi zitakazotolewa. Aidha amesema kuwa  kwa mwaka huu jumla ya wanafunzi 230 wamehitimu na kutunukiwa shahada mbalimbali na kati ya hao wanaume 104 na wanawake 126 ambao wametunukiwa astashahada, stashahada na shahada.

Amesema kuwa kwa Astashahada ya uuguzi wapo wahitimu 11, stashahada ya uuguzi wahitimu 21, shahada ya udaktari wa binadamu wahitimu 153, shahada ya uuguzi wahitimu 32, shahada ya uzalimili  ya ustawi wa jamii wahitimu 3, shahada ya uzamili wa sayansi ya afya ya jamii wahitimu 2, shahada ya uzamili ya magonjwa na afya za watoto wahitimu 5 na shahada ya uzamili ya Magonjwa ya akina mama wahitimu 3. Mgone amesema kuwa  na kwa mwaka huu wa masomo 2018/2019 wamedahili wanafunzi wapya 293 na chuo kimeendelea kufadhili masomo kwa walimu ngazi ya uzamili na uzamivu na hadi sasa wana walimu 4 wanaosomea shahada ya uzamivu na 3 shahada ya uzamili katika fani mbalimbali.
 Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki, John Ulanga akizungumza wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbali mbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Profesa Charles Mgone, akizungumza wakati wa kuhudhurisha na kutunuku wahitimu 230 waliohitimu mwaka huu ambapo ameeleza kuwa wana mpango wa kujenga kampasi mpya itakayoongeza idadi ya wanafunzi na kozi zitakazotolewa wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbali mbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam. (Picha na Bakari Madjeshi, Blogu ya jamii)
 Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Dkt. Salim Mohamed Salim (kulia) akiteta jambo na Makamu mkuu wa hicho hicho Profesa Charles Mgone wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbalimbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu waliotunukiwa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa mahafali ya 16 katika ngazi mbalimbali za uuguzi na udaktari yaliyofanyika leo Desemba Mosi, 2018 katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU

yaani makala yote UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/ujenzi-wa-kampasi-boko-kuongeza-idadi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UJENZI WA KAMPASI BOKO KUONGEZA IDADI YA KOZI HKMU"

Post a Comment