title : MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA
kiungo : MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA
MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA
Mradi wa Majitaka unaotekelezwa kwenye maeneo ya miinuko Jijini Mwanza unaofahamika kama "Simplified Sewerage" umekuwa miongoni mwa miradi miwili bora zaidi kuwahi kutekelezwa Barani Afrika chini ya ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF). Hayo yameelezwa mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2018 wakati wa Mkutano wa kujadili miradi inayofadhiliwa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kupitia mfuko huo wa EU-AITF.
Katika mkutano huo ilielezwa kwamba tangu mfuko huo uanzishwe mnamo mwaka 2007 ni miradi miwili pekee ambayo imefuzu na kuwa miradi bora zaidi kuwahi kutekelezwa ambayo ni Mradi wa Majitaka wa Simplified Sewerage wa Jijini Mwanza, nchini Tanzania na mwingine ni mradi wa Nishati ya Umeme wa Benin & Togo.
Akizungumzia mradi wa Majitaka wa Jijini Mwanza, Mshauri wa masuala ya Kiufundi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Raoul Pedrazzani alielezea hali ilivyokuwa hapo awali kabla ya kujengwa kwa mradi mpya wa majitaka kwenye maeneo ya milimani jijini humo. Pedrazzani alisema kuwa kijiografia maeneo mengi ya Jiji la Mwanza ni milima/miinuko na kabla ya mradi huo wa majitaka wakaazi wa maeneo ya milimani hawakuwa na mfumo mzuri wa uondoaji wa majitaka hali ambayo iliwasababishia adha mbalimbali ikiwemo uchafuzi wa mazingira na maradhi.
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akikagua ubunifu uliotumika katika ujenzi wa mradi wa majitaka, Mabatini mtaa wa Unguja wilaya ya Nyamagana. Mradi huo umejengwa kwenye maeneo ya miinuko na umesaidia kuondosha uchavuzi wa mazingira na magonjwa ikiwamo Kipindupindu.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (mbele) akiwaongoza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Mjini Moshi (MUWSA) eneo la Mabatini Jijini Mwanza walipotembelea kujifunza mfumo wa majitaka Oktoba, 2018. Ni mradi wa kipekee kuwahi kutekelezwa nchini.
Moja ya eneo lililonufaika na mfumo wa majitaka ujulikanao kama ‘Simplified Sewerage’. Pichani ni Mtaa wa Unguja, Kata ya Mabatini Jijini Mwanza ambao ni miongoni mwa maeneo yaliyonufaika na mradi wa majitaka wa simplified sewerage kupitia ufadhili wa African Infrastructure Trust Fund (EU-AITF).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA
yaani makala yote MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mradi-wa-majitaka-mwanza-waibuka-kinara.html
0 Response to "MRADI WA MAJITAKA MWANZA WAIBUKA KINARA"
Post a Comment