TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’

TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’ - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’
kiungo : TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’

soma pia


TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation linatarajia kufanya matamasha makubwa matatu jijini Dar es Salaam katikaa wilaya za Ilala, Temeke na Kinondoni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga, inayofanyika sambamba na kutoa burudani.

Hii ni kuunga mkono hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli siku ya tar 21 Juni 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega alisema tamasha hilo litapambwa na wasanii Shilole, Man Fongo, Belle 9, Dully Skykes pamoja na Chege Chigunda.

Alisema burudani hiyo itaanza siku ya Ijumaa Desemba 21, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala, na siku ya Jumamosi Desemba 22, Kampenii hizo zitafanyika Wilaya ya Ilala katika Uwanja wa Karume huku fainali za burudani hizo kumalizikia Jumapili Desemba 23, Wilayani Temeke katika Viwanja vya Mbagala Zakhem.

“…Hadi tunavyozungumza leo, Kampeni hii imetembelea Mikoa yote ya Tanzania Bara na Miji mashuhuri na Wikiendi hii ni zamu ya Jiji la Dar Es Salaam. Katika Kampeni za mikoani, tumefanya kazi na Wasanii wawili maarufu, Shilole na Man Fongo.


Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia matamasha matatu makubwa ya kampeni za ‘Rudi Nyumbani Kumenoga’ yatakayoanza Desemba 21, Kinondoni Uwanja wa CCM Mwinjuma- Mwananyamala, Desemba 22 Ilala katika Uwanja wa Karume na Desemba 23 Wilaya ya Temeke viwanja vya Mbagala Zakhem. Kushoto ni Afisa Masoko wa TTCL, Mohamed Shaaban pamoja na Afisa Masoko wa shirika hilo, Bi. Aurelia Boniface (kulia).
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, wakiwa katika mkutano huo.  


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’

yaani makala yote TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/ttcl-kuitikisha-dar-na-tamasha-la-rudi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TTCL KUITIKISHA DAR NA TAMASHA LA ‘RUDI NYUMBANI KUMENOGA’"

Post a Comment