TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti

TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti
kiungo : TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti

soma pia


TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti




Hussein Ndubikile
Mwamba wa Habari
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imewataka Mawakili wote kujisajili kwenye mamlaka hiyo ili waingizwe katika makusanyo ya Kodi ya Ongezeko ya Mapato(VAT) huku ikibainisha itaanzisha oparesheni ya kuwakamata wananchi ambao hawadai risiti wanapofanya manunuzi ya bidhaa.

Aidha, mamlaka hiyo imewataka mawakili kuhakikisha wanawasilisha kodi hiyo kila mwezi lengo likiwa kuongeza makusanyo ya mapato.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Abdul Mapembe wakati wa Semina iliyoikutanisha mamlaka hiyo na mawakili ikilenga kuondoa sintofahamu ya masuala ya kodi baina pande zote mbili pamoja na kukumbushana wajibu wa kulipa kodi.

Amesema kuwa mawakili wengi wamekuwa hawana utamaduni wa kujisajili TRA ili kulipia VAT hali inayosababisha mapato kupotea hivyo anaamini semina hiyo ni chachu ya kuwapa uelewa mawakili umuhimu wa kulipa kodi.

“Sheria inawataka mawakili kujisajili katika Kodi ya Ongezeko ya Mapato pia wanatakiwa kuwasilisha mapato sahihi ya mwaka,” amesema.

Amebainisha kuwa semina hiyo ni endelevu na kwamba mamlaka hiyo itaendelea kutoa elimu kwa mawakili wa mikoa mingine ikiwemo Mbeya, Arusha, Dodoma na Mwanza.

Amesisitiza kuwa katika semina hiyo mawakili wamewasilisha changamoto zao ikiwemo nyaraka za mikataba ya mauziano kutoaminiwa na TRA pamoja na za usajili.

Amefafanua kuwa wataanzisha oparesheni kabambe ya kuwakamata wale wote ambao hawadai risiti za bidhaa kwani vitendo hivyo vinaipotezea mapato mamlaka hiyo.

Katika hatua nyingine, amewataka wananchi kutoa taarifa za watu  wanaojihusisha na vitendo vya ukwepaji kodi ili wachukuliwe hatua stahiki.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani wa mamlaka hiyo, Abdul Zuberi amesema elimu iliyotolewa kwa mawakili hao itasaidia kuwafikishia wenzao ambao hawajajua umuhimu wa kujisajili kuingizwa kwenye VAT.

Naibu Kamishna Zuberi amewataka mawakili wawe mstari wa mbele wa kulipa kodi na kubainisha mambo yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi na mamlaka hiyo ili kuondoa changamoto zilizopo.

Naye Wakili, John Rugambo ameiomba TRA kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama ya mashine za Kielektroniki ili kuwavutia vijana na mawakili wanaotaka kuanza kufanya biashara.

Pia ameishauri mamlaka hiyo kuendesha mafunzo kwa watendaji wake kupunguza usumbufu wanaoupata wakati wakifutailia masuala mbalimbali.

Wakili Rugambo amependekeza mamlaka kutoa mashine za Efd bure na kuwalipisha kodi rafiki ya mapato ya mwaka.


Hivyo makala TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti

yaani makala yote TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tra-yawataka-mawakili-kujisajili-vat.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRA yawataka Mawakili Kujisajili VAT, kufanya oparesheni kukamata wananchi wasiodai risiti"

Post a Comment