TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030

TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030
kiungo : TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030

soma pia


TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MTANDAO wa ujinsia nchini (TNGP) umefanya mkutano na mjadala kuhusiana na haki ya afya ya uzazi uliowakutanisha wadau mbalimbali wanaofanya kazi katika sekta ya afya ikiwa ni katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Akizungumza katika mkutano huo Afisa programu wa wanaharakati na ujenzi wa pamoja (TNGP) Anna Sangai amesema kuwa lengo la kufanya mkutano huo ni kufanya tathimini ya wapi walipo na wanapoenda kuhusiana na hali ya jinsia nchini.

Akieleza tathimini ya nchi Sangai amesema kuwa Tanzania inafanya vizuri kiutekelezaji katika kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto. Pia ameeleza kuwa changamoto zinazozikabili mapambano hayo ni pamoja na kutofika kwa  elimu ya afya ya uzazi katika maeneo mbalimbali, utekelezaji wa sheria na mipango dhidi wanaovunja sheria na kufanya vitendo vya ukatili pamoja na mazingira magumu ya upatikanaji wa haki kwa kuwa kesi huchukua muda mrefu huku waathirika wakisumbuka kutafuta haki zao.

Sangai amesema kuwa mjadala huo utaweka mazingira wezeshi na kutoka na kampeni mbalimbali zitakazohusisha wadau  kutoka sekta ya afya nchini kote na hiyo itasaidia kufikia malengo  ya kupunguza asilimia 50 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ifikapo 2030. Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kuzuia unyanyasaji wa kijinsia, Sophia Komba amesema kuwa katika mkutano huo watazungumzia haki ya afya ya uzazi ambayo imekumbwa na na matukio ya unyanyasaji hasa kwa vijana na wanawake.
Afisa programu wa wanaharakati na ujenzi wa pamoja kutoka mtandao wa ujinsia nchini (TNGP) Anna Sangai akizungumza wakati wa mkutano huo uliolenga kujadili haki ya afya ya uzazi uliofanyika leo jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa wanaendelea na mikakati ya kufikia malengo ya kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia ifikapo 2030.
Mshauri wa masuala ya kijinsia kutoka Afrika kusini Kubi Rama akifafanua jambo katika mkutano uliolenga hasa kujadili haki ya afya ya uzazi  ulioandaliwa na mtandao wa ujinsia nchini (TNGP) na kueleza kuwa usawa lazima uwepo na kuzingatia kwa kuwa matukio mengi ya unyanyasaji hutokea pale ambapo mtu hukosa chanzo chochote cha kupata kipato hasa kwa wanawake.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kuzuia unyanyasaji wa kijinsia Sophia Komba akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam na kueleza matatizo ya ubakaji na kulawitiwa lazima yazungumzwe ili yaweze kukoma.
Mkutano ukiendelea

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030

yaani makala yote TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tngp-yazidi-kuendeleza-mikakati.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030"

Post a Comment