SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA

SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA
kiungo : SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA

soma pia


SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA

Serikali imewaonya watu wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwenye sekta ya Bima ya Afya nchini ikieleza kuwa mkono wa sheria hautawaacha salama.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Makampuni ya Bima ya Afya Tanzania (ATI), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile alisema kuwa Serikali inatambua kuwa udanganyifu huo hufanywa na baadhi ya watoa huduma za afya na watu wanaotibiwa kwa mfumo huo. Aliongeza kuwa wakati mwingine vitendo hivyo hufanywa kwa ushirikiano kati ya wafanyakazi wasio waaminifu pamoja na wateja.

Dkt. Ndugulile ametoa onyo kwa wanaojihusisha na udanganyifu kwa lengo la kuhujumu huduma za Bima ya Afya, kuwa kitendo hicho ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo jela pamoja na faini

“Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapinga kwa vitendo rushwa na udanganyifu; na yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo huchukuliwa hatua kali za kisheria. Serikali hii imeelekeza nguvu zake katika kujenga mfumo na taifa lenye uadilifu,” alisema.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi binafsi za bima ya afya, kwenye mkutano wa wadau wa Bima ya Afya nchini uliofanyika Jumatatu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile akipokea Cheti cha Shukurani kutoka Mwenyekiti wa Kamati ya Makampuni Binafsi ya Bima ya Afya, Bi. Violet Mordichai katika Mkutano wa wadau wa Bima ya Afya nchini, uliofanyika Jumatatu katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha  ya pamoja

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA

yaani makala yote SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/serikali-yaonya-wadanganyifu-kwenye.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA"

Post a Comment