title : SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI
kiungo : SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI
SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, ameiagiza Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi nchini (PSPTB), kuhakikisha kuwa inadhibiti maadili ya wafanyakazi wa sekta ya ununuzi na ugavi ili fedha za serikali zinazotumika kwenye ununuzi ziwe na tija kwa wananchi.
Bi. Mkapa ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo, wakati akifunga kongamano la tisa la wataalam wa ununuzi na ugavi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Bw. Mkumbo amebainisha kuwa licha ya vitengo vya matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia sekta ya ununuzi na ugavi, ikiwemo rushwa kuendelea kupungua, Bodi inatakiwa kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa vinadhibitiwa ipasavyo.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo, Bw. Richard Mkumbo, akifunga Kongamano la Tisa la Bodi ya Wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB), kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Susana Benard Mkapa, ukumbi wa DCC, Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPSTB), wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya kufunga kongamano hilo la siku tatu lililofanyika Jijini Dodoma na kuwashirikisha wataalam 650 kutoka Tanzania Bara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Sr. Dkt. Hellen Bandiho, akisoma hotuba ya ukaribisho kwa mgeni rasmi Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), iliyofanyika katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma
Kamishana wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Frederick Mwakibinga (kushoto), na mjumbe wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Dr. Laurent Shirima, wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo, wakati akifunga kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPSTB), wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo, wakati akifunga Kongamano la Tisa la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma.
Hivyo makala SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI
yaani makala yote SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/serikali-yaiagiza-bodi-ya-wataalam-wa.html
0 Response to "SERIKALI YAIAGIZA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI KUDHIBITI MAADILI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI"
Post a Comment