title : RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO
kiungo : RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO
RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO
Na. VERO IGNATUS, ARUMERU
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe John pombe magufuli anatazamia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru
Mradi huo uliotiliwa saini hivi karibuni utazinduliwa katika kijiji cha kimyaki majira ya saa nne asubuhi na baadae kuzungumza na wananchi katika kijiji cha mringarimga
Wakizungumzia hali ya maji mkazi wa eneo mringaringa Josephat Joshua amesema wakinamama wanalazimika kwenda kutafuatamaji ya kunywa kutoka mringaringa kilometa mbili katika sehemu inayoitwa njoro au kwa wavii.Wakati mwingine sisi wakina baba tunabakia na watoto nyumbani.
'' Wakinamama wanafuata maji, hadi arudi nyumbani anakuwa tayari amechoka sana kutokana na kufuta maji umbali wote huo bado majukumu mengine yanamsubiria"alisema Joshua.Kwa akizungumza kwa bi Miriam Zakayo amesema inawalazimu kutembea umbali mrefu na kushindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati
'' Maji tunayoayatumia ni ya mto nayo yanachukua muda mrefu hadi kufunguliwa kwa sababu wengine tunayatumia katika mifugo, mashamba, hivyo tukitaka maji ya kunywa tunayafuata mbali"alisema Miriam.Mkazi mwingine wa kijiji hicho Saning'o Lebang'ute Laizer amesema kwa ujio wa Rais Magufuli kwao ni neema kwani itawatatulia tatizo hilo sugu la maji safi, barabara na umeme
''Tunashukuru sana kwa kuja kutufikia kwetu ni neema, barabara, hii inawahudumia watu wa kimmyaki, Ilikiding' a na Sambasha, mradi wa umeme, ni fursa kwetu pia"alisema Laizer.
Mkazi wa kijiji cha mringarimga Miriam Zakayo akienda kufuata maji safi umbali wa km 2 kutoka kijiji cha Kimnyaki.Aidha katika kuhakikisha tatizo la upatikanaji safi na salama wilayani Arumeru linapungua ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John pombe magufuli leo anatarajia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru.
Mkazi wa kijiji cha mringarimga Miriam Zakayo akienda kufuata maji safi umbali wa km 2 kutoka kijiji cha Kimnyaki,katika kuhakikisha tatizo la upatikanaji safi na salama wilayani Arumeru,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John pombe magufuli anatarajia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru.
Pichani kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo na Wananchi wa Arumeru akiwa sambamba na
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro kwa pamoja wakimkaribisa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ziara rasmi ya kikazi katika wilaya ya Arumeru leo Jumapili katika kata ya Kimnyak na kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 ambavyo ni Sehemu ya Mradi mkubwa wa Maji Kwa Jiji la Arusha ambao utasaidia pia kutoa huduma ya Maji katika kata Saba za Wilaya ya Arumeru , Mradi utakuwa na thamani ya zaidi ya Bilioni 500.
Hivyo makala RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO
yaani makala yote RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/rais-dkt-magufuli-kuzindua-na-kuweka.html
0 Response to "RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO"
Post a Comment