PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI

PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI
kiungo : PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI

soma pia


PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI


Katika kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu kwa ufanisi zaidi taasisi ya Pamoja Foundation kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation imezindua hostel kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa shule za serikali.

Uzinduzi wa hostel hiyo uliogharimu jumla ya shilingi milioni 50 umefanywa leo na Diwani wa Kata ya Tuangoma Mohamed Suleiman kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Mbagala Ally Mangungu katika eneo la Mzinga wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hostel hiyo, Diwani wa Kata ya Tuangoma Selemani amepongeza ubunifu uliofanywa na taasisi ya Pamoja foundation kwa kuanzisha mradi wa kusaidia wasichana hasa katika masuala ya elimu na kuzitaka taasisi nyingine kushirikiana katika kusaidia masuala ya elimu ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.

Aidha, aliwaasa wananchi wengine kuiga mfano wa mwananchi wa eneo la Mzinga kwa kutoa eneo la wakfu kwa ajili ya kujengwa hostel hiyo ambapo alisema uamuzi huo utawezesha kujenga hostel nyingi na kubainisha kuwa eneo la Tuangoma ulipo mradi wa viwanja 20000 yeye kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Mbagala ataangalia namna ya kupata kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hostel kwa kuwa katika mradi huo kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya shule.

Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akifungua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli iliyojengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation.Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho. 
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akizungumza wakati wa uzinduzi wa Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam leo, hostel hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Kushoto kwa Diwani ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho. 
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman (kulia) akiangalia vitanda katika moja ya vyumba vya Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. Wa pili Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Pamoja Foundation Haji Mrisho. 
Diwani wa Kata ya Tuangoma iliyopo Mbagala Dar es Salaam Mohamed Suleiman akikata utepe kuzindua Hostel ya wanafunzi wa kike kwa shule za serikali iliyopo eneo la Mzinga kata ya Tuangoma Dar es Salaam, hosteli hiyo  imejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya kimataifa ya NAMA Foundation. 




Hivyo makala PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI

yaani makala yote PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/pamoja-foundation-yazindua-hostel-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PAMOJA FOUNDATION YAZINDUA HOSTEL YA WASICHANA KWA SHULE ZA SERIKALI"

Post a Comment