title : NAIBU MEYA ILALA WASHUKIA VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KULELEWA NA AKIMAMA.
kiungo : NAIBU MEYA ILALA WASHUKIA VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KULELEWA NA AKIMAMA.
NAIBU MEYA ILALA WASHUKIA VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KULELEWA NA AKIMAMA.
Mwambawahabari
Na. John Luhende
Hakuna ukombozi wa kiuchumi kama unaopatika katika vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na Vikoba, hasa katika watu wa maisha ya chini.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Said. Kumbilamoto alipokuwa mgeni rasmi katika kikundi cha vikoba cha Mkombozi Trust Fund, Cha jijini Dar es salaam,ambapo amewasisitiza wanakikundi hao kuchangamkia fursa za mikopo ya Halmashauri inayotolewa bila riba.
‘’Sisi kama Halmashauri tarehe 6 Januari mwaka 2019, itakuwandiyo mwisho wa kupokea vikundi vyote vilivyoomba kupewa mikopo ,tarehe 7 wataalamu watakaa kupitisha mikopo yote iliyoombwa ,mwamko bado ni mdogo naomba tusii acheipite fursa hii”Alisema
Aidha Kumbilamoto ametoa pongezi kwa makundi ya wanawake kwa kuwa na mwamko wa kuchangamkia fursa za mikopo huku akitoa changamotokwa vijana wa kiume kuacha utegemezi kwa akinamama badala yake wajitume kufanya kazi kwabidii.
‘’Nimeangalia uchukuaji wa mikopo na kuona akaimama wamefanya vizuri lakini tatizo liko kwa vijana wakiume sasa sijui wameridhika na kupiga mizinga? ama kulelewa na akina mama? Vijana fanyeni kazi acheni utegemezi”Alisema.
Akijibu Risala ya Kikundi hicho Kumbilamoto amesema atakisaidia kikundi hicho kupata Viti na Mizani, japo hakutaja lini atawapatia lakini amesema changamoto hizo amezichukua nakuahidi kushirikiana na kikundi hicho kukabili changamoto hizo.
Pamojana hayo Kmbilamoto amewahamasisha wananchi wakata ya Vingunguti kujiandaa kwa Machinji ya kisasa inayotarajiwa kujengwa na serikali ambapo amesema itaongeza fursa za kiuchumi .
‘’Huwezi kuwa na machijio ya kisasa ukakosa kuwa nakiwand cha kutengeza Soseji hizo nifursa wengine mtapika chakula ,pia tuna ene la pembeni ni la halmashauri tunaweza kuweka biashara nyingine na akiama mama wanaonyeshewa mvua pale nje nao tutawajengea ili waboreshe biashara zao pia changamkiaeni vitambulisho vya ujasiliamali ambavyo amevitoa Rais ”Alisema
Kwaupande wake Mwenyekiti wa kikundi cha mkombozi Trust Fund ,amesema baada ya sheri za fedha kubadilika na kutakiwa usaji wanaendelea na hatua za usajili ambapo ,nakuelezam kuwa tayari wanawanachama zaidi ya miatatu na ndani ya mwaka wameweza kutomikopo ya shilingi million 20.
Masema pamoja na Mafanikio waliyopata wanachangamoto ya wananchama kurejesha kurejesha mikopo, hawana izani ya kupima bidhaa wanazo uzia wao kwa wao,na wanaupungufu wa viti vya kukalia.
Pamoja na hayo wamemshukuru kwa moyo wake wa kujitoa na kusaidia jamii ikiwemo kikundi chao.
‘’Hakuna Diwani aliye wahi kununua Abullance kwa wananchi wake ispo kuwa Kumbilamoto huyu ni kiongozi anaye jali watu wake ‘’Alisema
Hivyo makala NAIBU MEYA ILALA WASHUKIA VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KULELEWA NA AKIMAMA.
yaani makala yote NAIBU MEYA ILALA WASHUKIA VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KULELEWA NA AKIMAMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU MEYA ILALA WASHUKIA VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KULELEWA NA AKIMAMA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/naibu-meya-ilala-washukia-vijana-wa.html
0 Response to "NAIBU MEYA ILALA WASHUKIA VIJANA WA KIUME WANAOPENDA KULELEWA NA AKIMAMA."
Post a Comment