title :
kiungo :
Na John Luhende
Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi amewataka watendaji katika wizara ya Ardhi ambao alikuwa amewahamisha akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, ambaowamerudi tena mkoani humo kwa njia ya kujigharamia uhamisho kuwa, atawahamishia wilaya zisizona na migogoro iwapo watabainika kurudi tena.
Aidha amewataka wananchi kuwa na vitambulisho vya utaifa (NIDA) kwaajili ya kupatiwa hati za Kielektroniki ambapo tayari zimeanza kutolewa katika wilaya ya za Kinondoni, na Ubungo baadaye katika Wilaya za Ilala Temeke, na Kigamboni.
"Wananchi na taka mtuelewe kuwa kwa sasa hatutatoa hati kwa mtu ambaye Hana kitambulisho hicho hata Patiwa hati" alisema.
Pamoja na hayo Lukuvi amewataka wananchi kote nchini kulipa kodi ya ardhi na Wale ambao hawatalipa kwa wakati watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuuzwa viwanja vyao.
"Kwa wale ambao hawahatalipia viwanja vyao vitauzwa na nimetoa muda hadi mwezi wa Pili mwishoni wale wote ambao wanamiliki viwanja katika miradi ya viwanja 20,000 waviendeleze"alisema kabla hawajanyang'anywa"alisema
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza katika mkutano huo amesema serikali inatatua migogoro ya ardhi Kinondoni ikiwa ni pamoja na kutekeleza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu 2015akiwa wilaya ni Kinondoni.
Amesema wananchi wa Kinondoni wataondokana na tatizo la migogoro ya ardhi kwa kuwa Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi amekuja kwaajili ya kumaliza kazi hiyo na kuwataka wananchi kuamini Serikali kwa kuwa inafanyakazi kwaajili yao.
Awali akimkaribisha mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mhe. Daniel Chongolo amesema, Kinondoni ina migogoro mingi ya ardhi ikiwemo Migogoro ya makundi, migogoro ya double a location, kukosekana kwa fidia, na migogoro ya mvutano kuhusu mipaka.
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/na-john-luhende-waziri-wa-ardhi-nyumba.html
0 Response to " "
Post a Comment