title : Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama.
kiungo : Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama.
Na Mwashungi Tahir. Maelezo,Zanzibar.
SHEHA wa Shehiya ya Kwa Mtumwajeni Rajab Ali Ngauchwa amewashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchimbaji wa msingi na kufukia mipira ya maji ili waweze kupata maji safi na salama na kuondosha tatizo sugu lilodumu kwa muda mrefu katika maeneo hayo.
Hayo ameyasema huko Nyerere Shehia ya Kwa Mtumwajeni wakati walipokuwa wameshiriki pamoja na Mwakilishi wa jimbo hilo kuchimba misingi na kufukia mipira kwa lengo la kuondokana na tatizo hili na badala yake kupata faraja hapo baadae .
Amesema mashirikiyano ni kitu kinachohimizwa katika kila sehemu , hivyo amefarijika sana na wananchi wake kwa kujitokeza kufanya adhma hiyo na kujua kwamba sasa tatizo hilo litaweza kuwaondokea katika shehiya hiyo.
Aidha alisema tatizo la maji safi na salama kwa muda mrefu katika shehiya hiyo hayapatikani kisima kipo ambacho kilichimbwa na viongozi waliyopita lakini kilikuwa hakitoi huduma kwa kipindi kirefu sasa.
Hivyo Mwakilishi wa jimbo hilo Rashid Makame Shamsi amewakabidhi mipira hiyo ya maji safi na salama roll tatu kwa lengo la kulitatua suala hilo ambalo wananchi hao wamefarajika na kumshukuru kiongozi huyo kwani kisima hicho kwa muda mrefu hakitoi huduma.
Nae Mwenyekiti ya kamati ya kisima Mwadini Shaabani Khatibu wa shehiya hiyo amesema wanatoa shukurani zao kwa mwalishi wa jimbo hilo kwa kuwakabidhi mipira hiyo na wameahidi wataitunza na kuitunza na kushughulikia vizuri kisima hicho .
Pia amewataka wanachi hao kuchangia kwa kuweka akiba ili pale inapotokea uharibifu wa mashine katika kisima hicho waweze kukidhi haja na vile vile kusaidia umeme ili huduma iweze kuendelea.
“Nawaomba wananchi tuweze kujipanga kwa kuchangia huduma hii ili tuweze kujiwekea akiba pale yakitokea matatizo tuweze kuyakabili ili huduma iendelee”. Alisema Mwenyekiti huyo.
Sambamba na hayo mwakilishi wa Jimbo hilo Rashid Makame Shamsi akiwa ni miongoni ya walioshiriki katika uchimbaji huo na amekabidhi mipira ya maji roll tatu na vifa a vya mifereji ambavyo vitu hivyo vyote thamani yake ni million moja na laki mbili.
Hivyo makala Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama.
yaani makala yote Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mwakilishi-wa-jimbo-la-magomeni-ashiri.html
0 Response to "Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Ashiri Katika Uchimbaji wa Uwekaji wa Mipira ya Maji Safi na Salama."
Post a Comment