title : MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA
kiungo : MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA
MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Migogoro ya ardhi katika kijiji cha magubike kata ya nzii wilaya ya iringa imebakia kkama historia baada ya mradi wa feed the future (LTA) kufanikiwa kupima ardhi na kuwakabidhi hatimiliki ya kimila kwa wananchi wa kijiji hicho.
Akizungumza wakatika wa kukabidhi hati hizo za kimila mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa alisema kuwa kutolewa kwa hatimikili za kimila kunamaliza migogoro ya ardhi kwa wananchi wote waliopata hati hizo.
“Sasa tunaelekea kipindi cha kilimo ambapo ndio kuna kesi nyingi za mipaka ya ardhi, hivyo uwepo wa mradi huu wa LTA umetusaidia kumaliza kabisa migogoro ya ardhi naomba kuchukua nafasi hii kwa niaba ya serikali kuwashukuru kwa kazi mliyoifanya” alisema Mhapa
Mhapa aliwaomba viongozi wa mradi wa LTA kuhakikisha wanapima vijiji vyote vya halmashauri ya wilaya ya Iringa ili kuondoa migogoro yote ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Kama serikali ikisema ipime ardhi yote ni kazi nzito,kazi hii ilitakiwa kufanywa na serkali kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu imekuwa tatizo kubwa kwa serikali hivyo lazima mpongezwe kwa kazi yenu mnayoifanya” alisema Mhapa

Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakati wa kukabidhi hati miliki za kimila kwa wananchi wa kijiji cha Magubike kilichopo kata ya Nzii mkoani Iringa

Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakimkabidhi hati mmoja wa wananchi wa kijiji cha Magubike

Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakicheza nyimbo za asili pamoja na wananchi wa kijiji cha Magubike wakati wa ugawaji wa hati za kimila.
Hivyo makala MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA
yaani makala yote MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mradi-wa-lta-wamaliza-migogoro-ya-ardhi.html
0 Response to "MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA"
Post a Comment