title : MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI
kiungo : MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI
MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco amewataka wanachama wa chama hicho wajiepushe na migogoro, makundi na majungu yasiyokuwa na tija kwa ustawi wa chama chao kwani yanaweza kusababisha mpasuko miongoni mwao.
Salim alitoa wito huo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na wajumbe katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Handeni ambapo alisema kwa sasa wanachama hao wanatakiwa kubadilika na kutokuipa nafasi kwani inaweza kurudisha nyuma maendeleo.
Alisema suala hilo limekuwa likimuumiza sana huku akiwataka wanachama kuhakikisha wanaachana nayo ili waweze kuunganisha nguvu za pamoja katika kukijenga chama chao ili kiendelee kuwa imara na kuendelea kuwatumikia watanzania.
“Ndugu zangu labda niwaambie kwamba mimi naumizwa sana na migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza kwani haina tija kwa ustawi wa chama chetu na inaweza kutugawa sisi hivyo niwatake msiipe nafasi kwenye maeneo yenu tuungane kwa pamoja tushirikiana kwa lengo la kuhakikisha haipewi nafasi “Alisema Mnec huyo.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco akizungumza na wajumbe cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Handeni wakati wa ziara yake ya kujitambulisha ambapo alisisitiza umoja na mshikamano itakayofanyika mkoa mzima wa Tanga.
Mjumbe wa Halmashauri ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia niMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco kushoto ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo
MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Godwin Gondwe akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Sehemu ya wanachama wa CCM wilayani Handeni wakimsikiliza MNEC
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco katiati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Handeni Salehe Kikweo.
Hivyo makala MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI
yaani makala yote MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mnec-ratco-akemea-makundimigogoro-kwa.html
0 Response to "MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI"
Post a Comment