KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO

KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO
kiungo : KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO

soma pia


KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Mtwara

Serikali imeagiza korosho zote inazonunua kwa wakulima kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko kuanza kubanguliwa nchini.

Agizo hilo la serikali limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 8 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Hasunga alisema kuwa Mkakati wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli ni kuwanufaisha wakulima nchini hivyo maamuzi ya kununua korosho ni sehemu ya maamuzi mema kwa manufaa ya wakulima wote.

Alisema wakati serikali inaendelea kukamilisha uhakiki wa wakulima wa korosho pamoja na kuendelea na malipo ya wakulima mpaka hivi sasa tayari wakulima 77,380 wamekwishalipwa hivyo hakuna korosho itakayoruhusiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi bila utaratibu maalumu badala yake korosho zote zitabanguliwa nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Kushoto ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) wakati wa Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. 
Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Joseph Buchweshaija na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakifatilia Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018



Hivyo makala KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO

yaani makala yote KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/korosho-zote-zitabanguliwa-nchini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO"

Post a Comment