title : Kampuni ya mabasi UDA RT yawakikishia Usalama wa kutosha Wananchi
kiungo : Kampuni ya mabasi UDA RT yawakikishia Usalama wa kutosha Wananchi
Kampuni ya mabasi UDA RT yawakikishia Usalama wa kutosha Wananchi
Na Heri Shaban
Mwambawahabari
KAMPUNI ya mabasi inayotoa huduma katika mabasi yaendayo haraka Dar es Salam RT imewatoa hofu Wananchi wa Mkoa huo na kuwakikishia Usalama wa kutosha katika mabasi hayo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji UDA RT John Nguya,wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Usalama wa mabasi hayo kufuatia mwishoni mwa wiki Gari la kampuni hiyo kutokea ajali ya moto iliyotokea na Itilafu katika mfumo wa umeme.
Nguya alisema mwishoni mwa wiki basi lao kubwa lenye uwezo wa kubeba abiria 155 Kimara kuelekea GEREZANI Kariakoo lilishika moto katika injini na kuwatia hofu Wananchi.
"Moto ulidhibitiwa na kwa ushirikiano wa Wananchi waliokuwa eneo la tukio pamoja na Jeshi la Zimamoto la Uokoaji, Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa UDA RT kwa kutumia vifaa vya kuzimia vilivyomo katika mabasi haya "alisema Nguya.
Aidha pia Nguya alisema abiria yoyote ambaye anasafiri ndani ya mabasi hayo Usalama wao upo wa kutosha kuanzia Mwanzo wa safari hadi mwisho safari na kila basi la Kampuni hiyo wataalam waliotengeneza wamefunga vifaa maalum vya kuzima moto vitatu vifaa hivyo vinafunguka wenyewe baada joto kuzidi na mabasi makubwa wamefunga vizima moto vinne vyenye ujazo wa klogram tatu na mlango mkubwa pande zote mbili kwa ajili ya dharura na matumizi.
Alisema Usalama wa mabasi hayo umethibitishwa kwa asilimia 100 kutokana na matengenezo yake yanatengenezwa kwa umahiri mkubwa na viwango vya kimataifa.
"Tunawakikishia Wananchi UDA RT inatoa kipaumbele kwa Usalama wa Watumishi wake,abiria wanatumia usafiri huo, watumiaji wengine wa barabara na vyombo vyake na tutaendelea kuchukua hatua za dhati ili kuzuia, kuepusha kukabiliana na dharura yoyote pindi inapojitokeza na kuendelea kutoa huduma kwa mujibu wa sheria na Usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara "alisema
Hivyo makala Kampuni ya mabasi UDA RT yawakikishia Usalama wa kutosha Wananchi
yaani makala yote Kampuni ya mabasi UDA RT yawakikishia Usalama wa kutosha Wananchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kampuni ya mabasi UDA RT yawakikishia Usalama wa kutosha Wananchi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/kampuni-ya-mabasi-uda-rt-yawakikishia.html
0 Response to "Kampuni ya mabasi UDA RT yawakikishia Usalama wa kutosha Wananchi"
Post a Comment