title : HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE
kiungo : HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE
HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE
*Pia wanne warejeshewa uanachama wao, yumo Madabiba
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
HALMASHAURI KUU ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), imetangaza kuwa mwanachama wake mpya Abdallah ,Mtolea ameteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam.
Kwa kukumbusha tu Mtolea kabla ya kujiunga CCM alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi(CUF) lakini siku za karibuni aliamua kujiondoa kwenye chama hicho na kujiunga na CCM ambapo
aliweka wazi amefurahishwa na jitihada za Rais Dk.John Magufuli katika kuwatumikia watanzania wote.
Akizungumzia maazimio ya Halmashauri Kuu, Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Alli amesema leo kuwa Mtolea amepitishwa kugombea ubunge kupitia chama hicho katika uchaguzi wa ubunge. "Kwa kauli moja
Halmashauri Kuu imepitisha jina la Abdallah Ali Mtolea kugombea ubunge kwenye jimbo hilo la Temeke."amesema Dk.Bashiru.
Wakati huo huo Dk.Bashiru amesema kuwa Halamshauri Kuu imempa kalipio kali mwanachama wao Hasnal Muruji kutokana na kukiuka maadili ndani ya chama hicho.Aidha Dk.Bashiru amezungumzia uamuzi wa Halmashauri Kuu wa kuwarejeshea uanachama wanachama wake wanne akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida.Wengine waliorejeshewa uanchama aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa, aliyekuwa
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Chistopher Sanya huku aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akiendelea kuwa chini ya uangalizi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari alipokuwa akizungumza nao leo Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam,kuhusu yaliyojiri katika vikao vikuu viwili vya chama ambavyo ni Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) vilivyofanyika kati ya tarehe 17 na 18 Desemba, 2018 Jijini Dar es Salaam.Vikao hivyo vimeongozwa na Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkuu Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa tayari kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally kwenye mkutano wake na Waandishi hao uliofanyika leo Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam
Hivyo makala HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE
yaani makala yote HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/halmashauri-kuu-yapitisha-jina-la.html
0 Response to "HALMASHAURI KUU YAPITISHA JINA LA MTOLEA KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE"
Post a Comment