title : DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI
kiungo : DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI
DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI
*Asema baadhi yao wapo wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi, adai anao ushahidi
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo amewahatahadharisha vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne ambao hawakubahatika kuendelea na masomo kuacha kujiunga na mafunzo ya kigaidi.
Kizigo aliyasema hayo kwenye kikao cha ushauri cha Wilaya ya Namtumbo kilichofanyika jana ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo amedai
kuwepo kwa ushahidi wa wazi wa jeshi la polisi ambao unadai wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na wale wanaomaliza kidato cha nne na kutobahatika kuendelea na masomo ndio wanaojiunga na mafunzo hayo ya ugaidi wilayani humo.Hata hivyo kupitia kikao hicho Mkuu wa wilaya huyo aliagiza wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne ambao hawatapata nafasi ya kuendelea na masomo na wanapohitajika na taasisi za kidini kwa kisingizio cha kwenda kufanya kazi lazima wapate kibali kutoka katika ofisi yake.
Kwa upande wa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) wilayani Namtumbo Rashidi Mfaume pamoja na kumpongeza mkuu wa wilaya kwa hatua hiyo lakini alimwomba kuwashirikisha wenyeviti wa serikali za mitaa na vitongoji katika utoaji wa vibali hivyo.Pamoja na hayo kikao hicho cha ushauri cha wilaya kilipitia muhtasari wa maadhimio ya mwaka 2016 ambapo adhimio la kuanzisha Wilaya ya Sasawala wajumbe walidai liindelee kufuatiliwa kulingana na umuhimu wake pamoja na adhimio la kuongezewa jimbo la Sasawala nalo lilibaki kama lilivyopitishwa katika kikao cha mwaka 2016.
Kuhusu azimio la kuyarudisha mashamba yanayomilikiwa na (NAFCO)Shirika la chakula la taifa ambayo kwa sasa hayaendelezwi yarudishwe kwa wananchi pamoja na shamba la Likenangena ambalo nalo awali lilionekana kumilikiwa na wizara ya fedha nalo haliendelezwi .
Mafunzo ya kigaidi wilayani humo yalibainika kufanywa katika misitu ya kijiji cha Mchomoro na Masuguru wilayani humo ambapo Jeshi la polisi Kwa umahiri wake walifanikiwa kuwakamata wahusika na kusambaratisha mafunzo hayo.
Hivyo makala DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI
yaani makala yote DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/dc-namtumbo-aonya-wanaojihusisha-na.html
0 Response to "DC NAMTUMBO AONYA WANAOJIHUSISHA NA MAFUNZO YA KIGAIDI"
Post a Comment