DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO

DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO
kiungo : DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO

soma pia


DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amezungumzia ziara ya kikazi ambayo imefanywa na Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa wilayani humo kwa lengo la kuangalia hali ya kilimo hasa kipindi hiki cha msimu wa kilimo kwa mwaka 2018 /2019.

Akizungumza na Michuzi Blog , Mkuu wa Wilaya Sophia Kizigo amesema Bashungwa akiwa kwenye wilaya hiyo alipata nafasi ya kuzungumza na wakulima kuhusu hali ya kilimo kwa mwaka huu, pia alipata nafasi ya kuangalia iwapo mbolea imefika kwa wakati au laa.

Kizigo amesema kwenye suala la mbolea, Naibu Waziri wa Kilimo alipata nafasi ya kwenda kwa wasambazaji wakubwa wa mbolea ambapo alikutambolea imefika kwa wakati na ipo ya kutosha na baada ya hapo akaenda kwawakulima ambako nako alikuta mbolea haina tatizo.

"Hata hivyo kwa wakulima wa tumbaku wao wamenunua na kuanza kuitumia mbolea bila tatizo, ila kwa wakulima wa mahindi wengi wao licha ya mbolea kufika kwa wakati wameshindwa kuinunua kutokana na changamoto yakifedha.Sababu kubwa ya kutokuwa na fedha ya kununulia imetokana na beiya mahindi kwa msimu uliopita kuwa chini kwani kilo ya mahindi ilifikia Sh.200.

"Hivyo wengi hawajanunua ingawa tayari wameshapanda mahindi,ila kinachoonekana watanunua mbolea kwa ajili ya kukuzia mahindi.Tunafahamu Wilaya ya Namtumbo inaongoza kwa kilimo na hasacha mahindi ambayo mengi yanatoka wilayani kwetu,"amesema Mkuu waWilaya Kizigo wakati anaelezea ziara hiyo ambayo imefanywa na Naibu Waziri wa Kilimo Bashungwa.

Pia amesema akiwa humo amepata nafasi ya kutembelea wakulima kwabaadhi ya kata na kujionea hari ya wakulima hao katika kuandaa mashamba yao ambapo wengi wao wameshapanda kwani tayari msimu wa kilimoulishaanza ndani ya wilaya hiyo.

Akizungumzia maandalizi ya kilimo wilayani humo ,Kizigo amesema amefurahishwa na juhudi ambazo zinafanywa na wakulima katika kuhakikisha wanautumia vema msimu huu kwa kuandaa mashamba mapemana kwamba wengi wao wameshapanda mbegu kwani msimu wa kilimo umeshaanza katika wilaya hiyo.
 MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo akiwa ameambatana na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kwa pamoja wakitembelea mashamba ya mahindi katika vijiji mbalimbali kikiwemo kijiji cha Namanguli,kata ya Luchili wilayani Namtumbo
 Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa  akimsikiliza mmoja wa wakulima alipokuwa akizungumza nae kuhusu suala la upatikanaji wa mbolea,masoko na namna kilimo cha mahindi kinavyokwenda,kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh Sophia Kizigo.
 Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akimsikiliza Afisa Kilimo wa Wilaya alipokuwa akizungumza nae kuhusu namna ya wakulima wa Mahindi wananvyoandaa mashamba yao na kwa kiwango gani wanavuna mazao yao,na kwamba Mkulima anatakiwa alime heka ngapi ili asipate hasara,ambapo Afisa huyo alieleza kuwa Mkulima ili asipate hasara katika kilimo chake anapaswa kulima heka nne ili apate faida.
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa  pichani kulia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh Kizigo na wadau wengine wakikagua Shamba la mahindi katika kijiji cha Suluti kata ya Namtumbo.
 Ukaguzi wa shamba la tumbaku katika kijiji cha Suluti kata ya Namtumbo
 Wananchi walisimamisha msafara wa Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa katika kata ya Luchili kijiji cha Namanguli wakitaka wasikilizwe kero zao.
 Ukaguzi wa maduka ya pembejeo kuangalia mwenendo wa biashara na bei elekezi kama inazingatiwa ulifanyika pia.


Hivyo makala DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO

yaani makala yote DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/dc-kizigo-azungumzia-ziara-ya-naibu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC KIZIGO AZUNGUMZIA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA KILIMO WILAYANI NAMTUMBO"

Post a Comment