title : BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA
kiungo : BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA
BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee kujadili namna ya kufungamanisha Kilimo na Viwanda.
Amesema kuwa kampuni hiyo inazalisha bia kwa wingi nchini Tanzania hivyo mazungumzo hayo yataongeza chachu na tija katika kuongeza masoko ya wakulima nchini.
Mhe Bashunwa ameyasema hayo leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam na kuhudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa sera na Mipango, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya usalama wa chakula, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao.
Wengine ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo (TADB) na Benki ya Uwekezaji (TIB), Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko, na Muwakilishi wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee.

Kikao kikiendelea

Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee akifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) kujadili namna ya kufungamanisha Kilimo na Viwanda nchini.
Hivyo makala BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA
yaani makala yote BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/bashungwa-akutana-na-tbl-kujadili-namna.html
0 Response to "BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA"
Post a Comment