title : WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA
kiungo : WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA
WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha maslahi ya watumishi wote wa umma wakiwemo wa kada ya afya kupitia Bodi ya Mishahara na Motisha baada ya kukamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi.
Amesema kukamilika kwa uhakiki huo wa taarifa za kiutumishi kwa watumishi wa umma kutaiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kupanga upya mishahara na motisha kwa watumishi.
Waziri Mkuu alitoa taarifa hiyo jana jioni (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na watumishi wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji miundombinu wa kituo hicho uliogharimu sh. milioni 500.
Alisema Serikali inaendelea kushughulikia maslahi ya watumishi, hivyo aliwataka waendelee kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. “Tunataka mwananchi akifika kwenye maeneo ya kutolea huduma apokelewe, asikilizwe na ahudumiwe.”
Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kujenga Zahanati katika kila kijiji kwa kuwa wilaya hiyo imebakisha vijiji 2 kati ya 52 kumalizia ujenzi huo.
Waziri Mkuu alisema kwa sasa wananchi wa Ushirombo hawana sababu ya kusafiri umbali mrefu hadi Geita mjini au wilayani Kahama kwa ajili ya kufuata huduma za afya kwa kuwa huduma zote zitakuwa zikipatikana kituoni hapo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka Jiwe la Msingi la Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe, Novemba 29, 2018. Kulia ni Mbunge wa Bukombe na Naibu waziri wa Madini, Doto Biteko na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya cha ushirombo wilayani Bukombe, Novemba 29, 2018.
Wanakwaya wa Ushirombo wakiimba wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia Mkutano wa hadhara kwenye Stendi ya Ushirombo, Novemba 29, 2018.
Bibi Mageni Simon akiwa mwenye furaha baada ya kujifungua katika mazigira safi na salama ya hospitali ya wilaya ya Geita ya Nzera iliyokaguliwa na kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Novemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA
yaani makala yote WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-mkuu-tutaboresha-maslahi-ya.html
0 Response to "WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA"
Post a Comment