title : WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE
kiungo : WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE
WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE
*Aagiza wakurugenzi wakuu wa NSSF, AZIMIO, Kamishna TRA wakutane.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach Kigamboni na kutamka kuwa amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaendelea kwenye eneo hilo.
Amewaagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu kampuni ya Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal wakutane na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ili wajadiliane namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi.
Waziri Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 12, 2018) ambapo baada ya kufika katika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi ya 7,000 alionesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.
“Kuna mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibiwa, tutakuja kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moja. Ulinzi lazima uimarishwe pande zote mbili za mradi huu eneo la ujenzi na eneo la kuhifadhia vifaa vya ujenzi.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Majengo ya DEGE ECO- VILLAGE mradi wa ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .jana Novemba 12/2018
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu atembelea DEGE ECO- VILLAGE mradi wa ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimio wa Nyumba 7,4460 zilizopo Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF .Wiliam Erio na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimio. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo jana Novemba 12/2018.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu atembelea DEGE ECO- VILLAGE mradi wa ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF Balozi Ali Siwa.na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimiao. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo jana Novemba 12/2018.
Hivyo makala WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE
yaani makala yote WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-mkuu-asikitishwa-wizi-kwenye.html
0 Response to "WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE"
Post a Comment