title : WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO 5 KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM
kiungo : WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO 5 KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM
WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO 5 KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amefanya ziara ya siku moja mkoani Dar es salaam, lengo la ziara hiyo ni kukagua miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko pamoja na kutaka kujua mikakati ya kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa mkoani humo ya kukabiliana na maafa hayo.
Katika ziara hiyo Waziri Mhagama emetembelea wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam hususan katika maeneo ambayo mkoa huo umeboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko. Maeneo hayo ni Jangwani, Mto Mbezi, Mto Ng’ombe, Mto Bungoni na mfereji wa Mtoni kwa Azizi Ally. Pamoja na kuridhishwa na jitihada zilizofanywa na mkoa wa Dar es salaam za kuboresha miundombinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko, pia na mikakati ya kukabiliana na maafa hayo waliyomueleza, Waziri Mhagama ametoa maagizo 5 kwa kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa ya mkoa huo kuyatekeleza ili menejimenti ya maafa ya mafuriko mkaoni Dares salaam iwe endelevu.
“Nimeridhishwa na juhudi zilizofanywa na serikali kuu chini ya uongozi wa Dkt.Joh Pombe Magufuli za kuboresha miundo mbinu ya kakabiliana na maafa ya mafuriko, na nimeona jinsi serikali ya ngazi ya mkoa na wilaya zote zinavyo jitahidi kujenga uwezo wa kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa. Pamoja na jitihada hizo ninge penda kuishauri na kuielekeza kamati na Mkuu wa mkoa ayasimamie maelekezo yangu.” Amesisitiza Mhagama
Mhagama ameiagiza Kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa kusimamia suala la uharibifu wa mazingira hususani maeneo ya mito na mabondeni kwa mujibu wa sheria ya menejimenti ya maafa ya mwaka 2015. Aidha alifafanua kuwa Maafa mengi ya mafuriko mkoani humo yanatokana na uharibifu wa mazingira unaochangiwa na ujenzi katika maeneno yasiyo stahili kama kingo za mito na mabondeni hali ambayo huzuia maji kutiririka na kusababisha mafuriko.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliye kuwa akimueleza juu ya ujenzi wa mfereji wa mto Ngo’mbe, wakati wa ziara yake ya kukagua miundo mbinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza, Bibi, Nuru Damson, mkazi wa Dar es Salaam, aliye kuwa akimueleza jinsi ujenzi wa mfereji wa mto Ngo’mbe, ulivyowasaidia kutopata athari za maafa ya mafuriko wakati wa ziara yake ya kukagua miundo mbinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa ujenzi wa miundombinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es saaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati wa ziara yake ya kukagua miundo mbinu hiyo mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO 5 KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM
yaani makala yote WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO 5 KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO 5 KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-mhagama-atoa-maagizo-5-kwa.html
0 Response to "WAZIRI MHAGAMA ATOA MAAGIZO 5 KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM"
Post a Comment