title : WAZIRI MAVUNDA AVIPIGA FAINI YA MILIONI I4.5 VIWANDA KWA KUKIUKA SHERIA ZA KAZI.
kiungo : WAZIRI MAVUNDA AVIPIGA FAINI YA MILIONI I4.5 VIWANDA KWA KUKIUKA SHERIA ZA KAZI.
WAZIRI MAVUNDA AVIPIGA FAINI YA MILIONI I4.5 VIWANDA KWA KUKIUKA SHERIA ZA KAZI.
Naibu Waziri Vijana, Ajira na Kazi Antony Mavunde amevitoza faini viwanda viwili jumla ya shillingi Million 14.5 kiwanda cha Silafrika na kiwanda cha Azania Group kutokana na kukiuka sheria za mahala pa kazi
Aidha, viwanda vilivyotozwa faini hiyo ni kiwanda cha Azania Group pamoja kiwanda cha kutengeneza bidhaa za plastiki Silafrika Tanzania kwa kutofuata sheria za kazi, namba 5 ya mwaka 2004.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema amevitoza faini viwanda hivyo kutokana na kukiuka sheria za kazi ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa vifaa kinga katika kampuni hizo.
Aidha ameipiga faini kampuni ya Azania jumla ya sh mill 9.5 kwa kutofuata sheria za masuala ya kazi kwa wafanyakazi wake ikiwemo kuwafanyisha kazi bila ya kuwa vifaa kinga pamoja na kutowapa mikaba ya kudumu.
Aidha amewaagiza maofisa kazi mkoa wa Dar es Salaam na Ofisa kazi Wilaya ya Temeke pamoja na wakala wa usalama mahala kazi, kukaa pamoja na wa ajira hao kupitia mikaba ya wafanyakazi hao ili kuhakikisha wanapata stahiki zao.
Hata hivyo, Mavunde amemtaka Mwajiri wa kampuni ya Azania kuhakikisha anawapatia mikataba na stahiki zao zote ikiwemo fedha za likizo,mifuko ya hifadhi jamii pamoja na kuwaunganisha katika vyama vya wafanyakazi
Akitoa malalamiko mbele ya Naibu Waziri Mavunde, mfanyakazi wa kampuni ya Silafrika, Hamis Ally amesema kuwa, Mwajiri wa kampuni hiyo amekua akiwafanyisha kazi bila kufuata utaratibu wa kazi ikiwemo kufanyishwa kazi zaidi ya masaa 12 bila malipo ya ziada.
Naye, Murshi Mahamoud ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Azania kwa zaidi 12 bila kuajiriwa, huku akiwataka analipwa sh 7000 kwa siku, ambapo amedai hafahamu chochote kuhusu sheria za kazi na ajira.
Amesema pamoja na maelekezo aliyoyatoa kwa kampuni hiyo, ameipiga faini jumla sh mill 5 kwa kukosa kua na vifaa kinga wala sanduku la huduma ya kwanza hali inayohatarisha usalama wa wafanyakazi wanapokua kazini.
Hivyo makala WAZIRI MAVUNDA AVIPIGA FAINI YA MILIONI I4.5 VIWANDA KWA KUKIUKA SHERIA ZA KAZI.
yaani makala yote WAZIRI MAVUNDA AVIPIGA FAINI YA MILIONI I4.5 VIWANDA KWA KUKIUKA SHERIA ZA KAZI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MAVUNDA AVIPIGA FAINI YA MILIONI I4.5 VIWANDA KWA KUKIUKA SHERIA ZA KAZI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-mavunda-avipiga-faini-ya-milioni.html
0 Response to "WAZIRI MAVUNDA AVIPIGA FAINI YA MILIONI I4.5 VIWANDA KWA KUKIUKA SHERIA ZA KAZI."
Post a Comment