title : WAZIRI DR MWAKYEMBE AWATAKA WADAU KUSAIDIA SANAA YA MAJUKWAANI(LIVE STAND UP COMEDY
kiungo : WAZIRI DR MWAKYEMBE AWATAKA WADAU KUSAIDIA SANAA YA MAJUKWAANI(LIVE STAND UP COMEDY
WAZIRI DR MWAKYEMBE AWATAKA WADAU KUSAIDIA SANAA YA MAJUKWAANI(LIVE STAND UP COMEDY
Mratibu wa Stand Up Comedy Angel Massaburi 'Chuchu' akipeanamkono na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe baada one shot la kikundi hicho walolipa jina la cheka bila kikomo.
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harisson Mwakyembe amewataka wadau kuweza kuwekeza kwa wasanii chipukizi ikiwa ni pamoja na Live Stand Up Comedy ambazo zimeanza kukubalika kwa jamii.
Mratibu wa Stand Up Comedy Angel Massaburi 'Chuchu'akiwa Jukwaani akichekesha hadhira , hadhira hapo pichani.
Mwakyembe aliyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi kwenye onyesho la Live Stand Up Comedy lililofanyika Tabata Segerea kwa muda wa masaa mawili huku wasanii wenye vipaji 10 wakionyesha uwezo wao na kufanikiwa kuvunja mbavu mashabiki.
Mratibu wa Stand Up Comedy Angel Massaburi 'Chuchu' na watano kutoka upande wa kulia anayefuata ni Dkt Harrison Mwakyembe, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa Sanaa za majukwaani baada ya one should katika ukumbi wa Luko Segerea Dar es salaam. (Picha zote na John Luhende).
"Nimewaona vijana wanaweza na nimefurahi kwa kuwa kupitia vichekesho wanatoa elimu wanaburudisha na kufanya usahau msongo wa mawazo, hivyo ni fursa nzuri kwa wadau wengine kuwekeza kwa kuwa tayari njia imeshaanza kuonekana hasa kwa wasanii hawa ambao wana uwezo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akitoa neno baada ya onesho.
"Mpango wa serikali ni kuweza kukuza kazi hizi za wasanii na kuwa nao bega kwa bega na kuna mikataba ambayo tutaingia na wadhamini kwa upande wa sanaa tutahakikisha wasanii wengine wanapata nafasi kufanya kazi nao ili waweze kuleta ushindani," alisema Mwakyembe.
Mratibu wa Stand Up Comedy Angel Massaburi 'Chuchu' amesema kuwa malengo yao ni kuweza kuitangaza bendera ya Tanzania kimataifa na uwepo wa Mwakyembe umewaongezea nguvu ya kupambana zaidi hasa kutokana na kazi ambazo wanazifanya .
"Sanaa inakua taratibu hivyo kazi yetu itafika mbali hasa kutokana na ushindani uliopo kwenye tasnia, kuna mambo mengi ya kufanya katika kazi yetu hasa ukizingatia kwamba kuchekesha mtu sio jambo jepesi kama wengi wanavyofikiria, tutaendelea kujituma na kufanya kazi nyingi zaidi," alisema Chuhu.
Hivyo makala WAZIRI DR MWAKYEMBE AWATAKA WADAU KUSAIDIA SANAA YA MAJUKWAANI(LIVE STAND UP COMEDY
yaani makala yote WAZIRI DR MWAKYEMBE AWATAKA WADAU KUSAIDIA SANAA YA MAJUKWAANI(LIVE STAND UP COMEDY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI DR MWAKYEMBE AWATAKA WADAU KUSAIDIA SANAA YA MAJUKWAANI(LIVE STAND UP COMEDY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-dr-mwakyembe-awataka-wadau.html
0 Response to "WAZIRI DR MWAKYEMBE AWATAKA WADAU KUSAIDIA SANAA YA MAJUKWAANI(LIVE STAND UP COMEDY"
Post a Comment