title : WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO
kiungo : WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO
WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wanaoishi katika hosteli za nje ya chuo hicho wako kwenye mazingira hatarishi kutokana na baadhi yao kufanyiwa vitendo vya kinyama huku ikidaiwa wengine tayari wamepoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.
Matukio mengine yanayotajwa kuwafika Wanafunzi hao ni pamoja na kuvamiwa na kuporwa mali ,kujeruhiwa kwa kuchomwa visu na kupigwa hasa kwa wanafunzi wa jinsia ya Kike jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limechangia baadhi yao kuathirika kimasomo na hata kupunguza hali ya kuendelea na masomo.
Kutokana na hali hiyo, Wahitimu wa Chuo hicho kuanzia mwaka 1963 wameanza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1000 ili kupunguza changamoto zilizopo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Harambee hiyo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira amesema miundombinu ya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi haikidhi mahitaji ya sasa na ya baadae kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kwamba kwa kiasi kikubwa inahitaji kuboreshwa.
Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira wakati wa uzinduzi ya kuchanga ujenzi wa Miundombinu ikiwemo Hosteli katika chuo hicho. Hivyo makala WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO
yaani makala yote WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waliomaliza-chuo-kikuu-cha-ushirika.html
0 Response to "WALIOMALIZA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI WAHAMASISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA CHUO HICO"
Post a Comment