title : WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO
kiungo : WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO
WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO
Na Stella Kalinga, Simiyu.
Kuelekea katika kipindi cha maandalizi ya bajeti ya mwaka 2019/2020 wito umetolewa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu na maeneo mengine kote nchini kuyapa kipaumbele masuala ya Lishe katika mipango na bajeti za Halmashauri zao, ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele wakati mafunzo maalum yaliyotolewa kwa baadhi ya viongozi na maafisa Lishe, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Kihwele amesema takribani asilimia 34 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima wana udumavu, hivyo ipo haja ya kutilia mkazo suala la lishe ili kutoathiri maendeleo ya ukuaji wa watoto, uwezo wao wa kufikiri na maendeleo yao kitaaluma(shuleni).
“Asilimia 34 ya watoto wa nchi nzima wenye umri chini ya miaka mitano wana utapiamlo, suala hili linaathiri sana watoto, mfano matokeo yao shuleni na uwezo wa kufikiri, ndio maana serikali imeweka lishe kama kipaumbele na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama wasimamizi tunapita kwenye Halmashauri nchi nzima kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya lishe katika bajeti ya mwaka 2019/2020” alisema.
Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele akizungumza na baadhi ya viongozi na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa akiwasilisha mada kuhusu mipango na bajeti ya masuala ya lishe Mkoani Simiyu kwa baadhi ya viongozi na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Kai.B. Mbaruk akizungumza na baadhi ya viongozi na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
Hivyo makala WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO
yaani makala yote WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/wakurugenzi-watakiwa-kuzingatia-afua-za.html
0 Response to "WAKURUGENZI WATAKIWA KUZINGATIA AFUA ZA LISHE KATIKA BAJETI ZA HALMASHAURI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO"
Post a Comment