title : Waitara awataka Wenyeviti na Madiwani kwenda na kasi ya JPM
kiungo : Waitara awataka Wenyeviti na Madiwani kwenda na kasi ya JPM
Waitara awataka Wenyeviti na Madiwani kwenda na kasi ya JPM
NA HERI SHAABAN
Mwambawahabari
Madiwani na Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa nchini watakiwa kusimamia majukumu yao ya kazi na kwenda na kasi ya Rais John Magufuli katika kuleta maendeleo.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI )Mwita Waitara wakati wa mkutano wake na wananchi wa kata ya Kipunguni Jimbo la Ukonga Wilayani Ilala Dar es Salaam leo.
"Madiwani na Wenyeviti mmechaguliwa na wananchi kama wawakilishi nataka mlete maendeleo katika maeneo yenu nchini mwende na kasi ya JPM serikali ya awamu ya tano kila kiongozi anatakiwa kuwajibika " alisema Waitara
Waitara alisema kiongozi yoyote ambaye atashindwa kutimiza wajibu wake katika kutatua changamoto za wananchi katika serikali ya awamu ya tano hafai inatakiwa kuomba likizo kukaa pembeni kuwapisha wengine.
Alisema pia katika jambo la maendeleo inatakiwa kuitisha vikao kuwashirikisha wananchi wao kupanga pamoja katika miradi wanayokubaliana.
Katika hatua nyingine Waitara amepiga marufuku michango kwa wanafunzi nchini wa shule za msingi na Sekondari.
"Mimi kama mwakilishi wa Rais nimeelekezwa na bosi wangu Seleman Jaffo nisimamie elimu na mwenzangu atasimamia upande wa afya hivyo marufuku michango kwa wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na Kidato cha kwanza" alisema
Akielezea changamoto za Kata ya Kipunguni Jimbo la Ukonga alisema Barabara ya Diwani Bombambili ujenzi wake unatarajia kuanza hivi karibuni mpaka Nyeburu Wakala wa Barabara TARURA watajenga na fedha zilizotengwa Bilioni 6.
Kuhusu changamoto ya maji Kipunguni yanatarajia kufika wakati wowote na suala huduma ya afya Serikali tayari imetenga shilingi milioni 700 kwa ajili ya hospitali ya Wilaya eneo la Kivule.
Aidha pia alielezea mikopo ya asilimia 10 ya Wanawake,Vijana na Walemavu alisema wananchi wote itawafikia mikopo hiyo wale waliokamilisha taratibu za usajili na Watendaji watakaokwamisha zoezi hilo watachukuliwa hatua.
Hivyo makala Waitara awataka Wenyeviti na Madiwani kwenda na kasi ya JPM
yaani makala yote Waitara awataka Wenyeviti na Madiwani kwenda na kasi ya JPM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waitara awataka Wenyeviti na Madiwani kwenda na kasi ya JPM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waitara-awataka-wenyeviti-na-madiwani.html
0 Response to "Waitara awataka Wenyeviti na Madiwani kwenda na kasi ya JPM"
Post a Comment