title : WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
kiungo : WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefanikiwa kupata dhamana baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi kuridhia wapate dhamana na kuwapangia masharti ya dhamana.
Hatua hiyo imekuja baada ya washtakiwa kupitia mawakili wao kupeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu kwa kuwa washtakiwa wameshtakiwa chini ya sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo kesi hizo zinasikilizwa Mahakama Kuu.
Washtakiwa waliopata dhamana ni Ofisa wa Mazingira NEMC, Deusdith Katwale(38) na Mtaalam wa IT NEMC, Luciana Lawi(33) wote wakazi wa Ubungo Msewe, Katibu Muhasi wa NEMC (Sekretari), Edna Lutanjuka (51) Mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, Msaidizi wa ofisa Mwaruka Mwaruka (42) na Ofisa mazingira Nemc, Lilian Laizer (27) wote wakazi wa Ukonga Mombasa.
Washitakiwa hao Octoba31, Mwaka huu walisomewa mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa Mazingira.
Akiwasomea masharti sita ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama Kuu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando amewataka kila mshtakiwa kuweka fedha benki kiasi cha Sh. Milioni 13.3 au kuwasilisha mahakamani hapo hati ya mali isiyoamisha yenye thamani hiyo ya fedha.
Hivyo makala WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
yaani makala yote WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/wafanyakazi-watano-nemc-wapata-dhamana.html
0 Response to "WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI"
Post a Comment