title : WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA
kiungo : WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA
WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA
WACHORAJI wa jengo jipya la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, wametakiwa kuharakisha ili serikali itangaze zabuni ujenzi uanze haraka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema jana mkoani hapa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kiwanja hicho ambayo ipo kwenye maboresho makubwa.
Mhe. Kamwelwe amesema kukamilika kwa michoro hiyo ya jengo la kisasa kutasaidia serikali kupitia wasimamizi wa ujenzi huo Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kutangaza zabuni na kupatikana kwa mkandarasi atakayejenga jengo hilo. “Kiwanja cha ndege kinashughuli nyingi na jengo la abiria ni kityu muhimu sana, hivyo ninaharakisha hao wachoraji wajitahidi kufanya haraka ili kukamilisha michoro hiyo,” amesisitiza Mhe. Waziri.
Hatahivyo, amesema ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa jengo la mizigo ambalo lipo mita chache kutoka eneo la abiria, ambapo ndege za mizigo zimejengewa maegesho yake rasmi tofauti na awali zilikuwa zikishusha upande wa ndege za abiria. Halikadhalika ametembelea jengo la kisasa la kuongozea ndege, ambalo nalo limekamilika kwa asilimia 90 na kuridhishwa na utendaji wa Mhandisi Mkazi, Godfrey Asulumenye wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, pamoja na eneo linapojengwa rada.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe jana akipata maelezo ya ujenzi wa Jengo la mizigo la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, Geofrey Asulumenye (aliyenyoosha mkono. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema.
Baadhi ya vyumba katika jengo la mizigo la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza ambalo linaendelea kujengwa, jana Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alitembelea na kuridhika na maendeleo ya ujenzi.
Mhandisi Simon Makoye (mwenye kofia ngumu), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), mchoro wa eneo linapojengwa rada, jana alipotembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayoendelea kwenye Kiwanja cha Ndege cha Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akimsikiliza Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, Geofrey Asulumenye (kushoto) wakatii akimpa maelezo mbalimbali ya ujenzi wa Jengo la kuongozea ndege la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza wakati alipofanya ziara jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) YA Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (kulia), akiongozana na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Rubilya wakiambatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe aliyetembelea kukagua maendeleo ya miradi kwenye kiwanja cha Ndege cha Mwanza. PICHA ZOTE KWA HISANI YA TAA .
Hivyo makala WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA
yaani makala yote WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/wachoraji-jengo-la-abiria-mwanza.html
0 Response to "WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA"
Post a Comment