title : VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA
kiungo : VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA
VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KAMPUNI ya Vodacom kwa kishirikiana na benki ya Commercial Bank of Afrika (CBA) wametangaza rasmi kampeni ya shinda na M -pawa itakayowasaidia wateja kujishindia zawadi kemkem.
Akimwakilisha Mkurugenzi wa benki ya CBA, Mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo Julius Konyani amesema kuwa wateja watakaoweka amana, kukopa na kulipa kwa wakati ndani ya wiki 6 kuanzia Novemba 1 watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
Amesema kuwa wateja 200 watakaopatika ndani ya wiki 6 ambao huweka amana katika akaunti zao za M-pawa watashinda mara mbili ya amana walizoweka.Aidha amesema kuwa wateja 15 wanaokopa na kulipa kwa wakati watazawadiwa kiasi cha shilingi laki moja na kwa wiki 6 jumla ya wateja 96 watanufaika na zawadi hizo.
Konyani amesema kuwa droo kubwa itakayochezeshwa mwishoni kabisa jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 100 zitatolewa, na hizo ni pamoja na bajaji tano zitakazotolewa kwa wateja watano ambao hukopa na kulipa kwa wakati kupitia M-pawa na mteja wa jumla atapata zawadi nono ya shilingi milioni 10.
Kwa upande wake Meneja masoko wa kampuni ya Vodacom Noel Mazoya amesema kuwa wao na washirika wao ambao ni benki ya CBA wataendelea kuleta karibu huduma za kijamii kwa mfumo wa kidigitali.Amesema kuwa hadi sasa wamewafikia zaidi ya wateja milioni 7 ambao wanatumia huduma ya Mpawa katika kuweka faida na kukopa na kwa usalama zaidi.
Mazoya amesema kuwa wateja wa Vodacom waendelee kutumia huduma hiyo ili waweze kunufaika na zawadi zinazotolewa na kampuni hiyo.
Meneja Masoko wa Vodacom,Noel Mazoya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wateja wa mtandao huo waendele kutumia ili waweze kunufaika na zawadi zinazotolewa.kulia ni Mwakilishi wa Meneja wa CBA,Julius Konyani (Picha na Emmanuel Massaka MMG).
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa CBA,Julius Konyani wa (kwanza kulia) akishangilia mara baada ya kupatikana ya mshindi katika droo iliyochezeshwa leo jiji Dar es Salaam.
Hivyo makala VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA
yaani makala yote VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/vodacom-kutoa-zawadi-kwa-wateja-wake.html
0 Response to "VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA"
Post a Comment