VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA
kiungo : VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

soma pia


VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

Na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali imesema kuwa vikundi vya Upatu havitasimamiwa chini ya Sheria mpya ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 (The Microfinance Act, 2018)kwa sababu havijihusishi na biashara ya huduma ndogo za fedha.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akihitimisha hoja za mjadala waMuswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.

Dkt. Mpango alisema Sheria hiyo itahusisha taasisi kama vile Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), Taassi za huduma ndogo za fedha zisizopokea na zinazopokea amana na vikundi vya kifedha vya kijamii, wakopeshaji binafsi na asasi za kijamii.

Alieleza kuwa Sheria hiyo pia inalenga kuwalinda wananchi wanaotegemea sekta ndogo ya fedha katika kuendesha maisha yao na shughuli za kiuchumi kwa ujumla na itasimamia na kudhibiti biashara ya huduma ndogo za fedha, kuwawezesha watumiaji na watoa huduma hiyo pamoja na kudhibiti changamoto zinazoweza kutokea katika sekta hiyo.

“Madhumuni ya Sheria hiyo ni kuwatambua watoa huduma ndogo za fedha kwa lengo la kuwasimamia, kupata takwimu, kuwalinda na kuwawezesha watumiaji wa huduma ndogo za fedha”, alisema Waziri Mpango.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi, akijibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni, Jijini Dodoma. Walioketi kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katikati, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi(kushoto) wakigonga meza kuashiria kuunga mkono hoja wakati wa kujibu hoja za Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma, kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akifuatilia kwa makini hoja hizo
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kushoto, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kulia, wakiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi (katikati) wakati wa kujibu hoja za Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, bungeni Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).



Hivyo makala VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

yaani makala yote VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/vikundi-vya-upatu-kutosimamiwa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA"

Post a Comment