title : UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA
kiungo : UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA
UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili wafanyakazi watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali, Jenipher Massue aamedai hayo leo Novemba 28.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando wakati kai hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa,
"Mheshimiwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa upelezi bado haujakamilika tu naomba tarehe ya kutajwa" amedai wakili Massue.
Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 12, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Katika kesi hiyo wafanyakazi hao wanakabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Januari Makamba katika vyeti vya tathmini ya uharibifu wa Mazingira.
Washtakiwa hao ni Ofisa wa Mazingira NEMC,Deusdith Katwale(38) na Mtaalam wa IT, Luciana Lawi(33) wote wakazi wa ubungo Msewe, Katibu Muhasi wa NEMC (Sekretari), Edna Lutanjuka (51) Mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, Msaidizi wa ofisa Mwaruka Mwaruka (42) naOfisa mazingira Nemc, Lilian Laizer (27) wote Wa kazi wa Ukonga Mombasa na Ofisa mazingira wa Nemc, Magori Wambura (38) mkazi wa Bombambili.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwamo la kula njama, mawili ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kusababisha hasara ya Sh.Milioni 160
Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Septemba 27, 2016 na April Mosi,2018 jijini Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa la kughushi.
Hivyo makala UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA
yaani makala yote UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/upelelezi-kesi-ya-uhujumu-uchumi.html
0 Response to "UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI WAFANYAKAZI WA NEMC BADO HAUJAKAMILIKA"
Post a Comment