title : TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA
kiungo : TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA
TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo (ASLMs) na wadau wa kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme Phase Two-ASDPII).
Katika utekelezaji wa ASDP II serikali imelenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo (mazao, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha na usalama wa chakula na lishe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 26 Novemba 2018 wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania inayofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam.
Alisema Utekelezaji wa lengo hilo ni kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula; kuimarisha uchumi; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda; na kuongeza ajira ambapo ili kufikia malengo hayo; Utekelezaji wa ASDP II utazingatia mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima na wafugaji na kwa bei nafuu.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza umuhimu wa sekta binafsi nchini wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya Wadau wa Kilimo na Mifugo nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua bidhaa zilizoongezwa thamani ndani ya nchi wakati wa hafla ya warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018. Kulia ni Maryam Issa mtendaji wa Kampuni ya NatureRipe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018.
Hivyo makala TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA
yaani makala yote TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/tumekusudia-kufanya-mageuzi-makubwa.html
0 Response to "TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA"
Post a Comment