title : TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU
kiungo : TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU
TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU
*Waziri Mkuu akabidhi majina hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa hatua
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela orodha ya matrafiki wanaodaiwa kuwaomba rushwa madereva wa noah wilayani Lushoto.
Majina ya trafiki hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa madereva wa noah wanaofanya kazi ya kusafirisha abiria ndani ya wilaya hiyo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu kupitia mabango.
Waziri Mkuu alimkabidhi majina hayo jana jioni (Jumatano, Oktoba 31, 2018) baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sabasaba, Lushoto mjini.
Baada ya kumkabidhi majina hayo alimuagiza afanye uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili askari hao na kisha awasilishe taarifa kwake leo Alhamisi Novemba 1, 2018.
Mbali ya wananchi kuwasilisha malalamiko hayo, Pia mbunge wa Lushoto, Shaaban Shekilindi alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kutatua kero hiyo inayowakabili wananchi.
Awali, Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Lushoto katika ukumbi wa chuo cha Mahakama Lushoto ambapo aliwasisitiza wafanye kazi kwa bidii.
Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haina msamaha na mtumishi wa umma asiyetaka kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa CCM Sabasaba uliopo Lushoto, Oktoba 31, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa Lushoto wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa CCM Sabasaba akiwa katika ziara ya mkoa wa Tanga Oktoba 31, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU
yaani makala yote TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/trafiki-waomba-rushwa-washtakiwa-kwa.html
0 Response to "TRAFIKI WAOMBA RUSHWA WASHTAKIWA KWA WAZIRI MKUU"
Post a Comment