title : TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO
kiungo : TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO
TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA cha Wanasheria Wanawake(TAWLA) kimewakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili , kuchambua na kuweka mikakati ya namna ya kuwasaidia watoto ambao wapo kwenye ukinzani wa kisheria hasa kipindi hiki ambacho mmomonyo wa maadili kwenye jamii umekuwa mkubwa na kusababisha watoto wengi kujikuta wakiingia kwenye ukinzani huo wa kisheria.
Baadhi ya wadau ambao wamekutanishwa na TAWLA ni polisi, maofisa ustawi wa jami, wanasheria wenyewe, mahakimu, masheikh na wachungaji pamoja na wadau wengine wanaojihusisha na masuala ya watoto nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA)Tike Mwambipile amesema wameamua kukaa pamoja na kisha kutazama nini wafanye katika kuwasaidia watoto walioko kwenye ushindani wa kisheria na kwamba wakati wa najadiliana kwenye hilo watatumia nafasi hiyo kuulizana maswali ya msingi ya kisheria likiwamo la wapi wamekosea.
Amefafanua sheria inasema kesi ya mtoto isikilizwe ndani ya siku mmoja na hiyo ni changamoto kwani ni ngumu kutumia siku moja kusikiliza kesi ambapo utahitaji pia mashahidi na mambo mengine ya kisheria na hivyo wadau hao wataangalia nini kifanyike angalau kutoa nafasi ya kutosha ya kusikiliza kesi za watoto kwenye makosa ya haki jinai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na chama hicho kujadili haki za Watoto wenye matatizo ambao wanahitaji msaada wa kisheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile akisoma moja ya Kitabu kinachohusu masuala ya kisheria wakati wa semina ya kujadili namna ya kumsaidia mtoto ambaye ameingia kwenye ukinzani wa kisheria.Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wakili Barnabas Kaniki akizungumzia mjadala ulioandaliwa na Chama hicho, uliokuwa unajadili haki za watoto wenye matatizo ambao wanahitaji masaada wakisheria.
Baadhi ya washiriki wa mjadala huo wakiwa kwenye semina maalum iliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA) walipokutaa leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO
yaani makala yote TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/tawla-yawakutanisha-wadau-kujadili.html
0 Response to "TAWLA YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA KISHERIA ZINAYOMHUSU WATOTO"
Post a Comment