SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA

SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA
kiungo : SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA

soma pia


SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA

Na Stella Kalinga, Simiyu
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  amezindua rasmi mfumo wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kupitia kwa mshitiri mmoja wa mkoa ujulikanao kama JAZIA, uliobuniwa kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Akizindua mfumo huo Novemba 05, 2018  Sagini amesema mfumo wa JAZIA si mbadala wa Bohari ya Dawa (MSD) bali unalenga kuziba upungufu wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika Bohari ya Dawa (MSD).

“JAZIA ni mfumo uliobuniwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wataalam washauri ili kuweza kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, JAZIA si mbadala wa MSD bali ni msaidizi wa MSD inapokuwa haina bidhaa husika.” alisema.

Aidha, Sagini alibainisha kuwa mfumo huu utasaidia kupunguza gharama na bei ya upatikanaji wa dawa kwani bei za dawa na vifaa tiba zitalingana na bei ya soko na sio matakwa binafsi ya wazabuni.

Aliongeza kuwa mfumo huo utapunguza urasimu uliokuwepo wa namna ya kununua dawa nje ya MSD na hivyo kusaidia dawa kupatikana kwa muda mfupi huku akiwataka Waganga wafawidhi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya kuagiza dawa na vifaa tiba mapema wanapoona vinapungua kabla ya kusubiri vifaa hivyo na dawa kuisha kabisa.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) akisaini mkataba wa mshitiri mmoja wa Mkoa katika dawa na Vifaa Tiba(JAZIA), Novemba 05, 2018  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi, waliosimama kushuhudia ni Baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu.
 Mkurugenzi wa Operesheni kutoka Kampuni ya Total Health Lab ya jijini Dar es salaam ,  Crispin Mtete na Mkurugenzi wa Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki wakisaii mkataba kama wazabuni walioungana kama mshitiri mmoja wa mkoa wa Simiyu katika kutoa huduma za dawa na vifaa tiba , Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
 Mkurugenzi wa Mufuruki Traders Company Ltd ya jijini Mwanza, Khalifa Mufuruki akizungumza jambo katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, ASF. James John akichangia hoja katika uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.
 Viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa mshitiri mmoja wa mkoa katika dawa na vifaa  tiba “ JAZIA” uliofanyika Novemba 05, 2018 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu Mjini Bariadi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA

yaani makala yote SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/simiyu-yazindua-mfumo-wa-mshitiri-mmoja.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA"

Post a Comment