SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI

SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI
kiungo : SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI

soma pia


SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI

Na Asteria Muhozya, Songea 

Serikali imesema haijaruhusu uchimbaji wa Madini katika Mto Muhuwesi na kwamba tayari Wizara ya Madini ilikwishakutoa maelekezo yapatayo matano ambayo wahusika wanatakiwa kuyafanyia kazi ili itoe maamuzi. 

Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea, wakati akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ambaye alimwomba Waziri asimamishe uchimbaji huo na kwamba tayari Mkoa umezuia shughuli hizo kuendelea kwa kuwa ndiyo chanzo cha maji mkoani humo na kwamba, alifanya hivyo ili kulinda miundombinu ya barabara. 

Waziri Kairuki alimweleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa, wizara ilitoa maelekezo kwa wahusika kwamba wanatakiwa kuwasilisha barua ya ridhaa ya Waziri wa Maji, ridhaa ya Wakala wa Barabara nchini (TANROAD), ridhaa ya Bodi ya Bonde la Mto Ruvuma/Pwani na Kusini ili wizara ijiridhishe kabla ya kutoa maamuzi. 

“ Tunataka tujiridhishe na approval kutoka katika maeneo hayo na vikipatikana vyote, nitafanya uamuzi. Kwa sasa ipo ridhaa ya bodi ya bonde la mto Ruvuma,” alisisitiza Waziri Kairuki 

Pia, akifafanua kuhusu kusimama kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya Uranium unaofanywa na Kampuni ya Mantra Tanzania Limited, waziri Kairuki alisema kuwa, kampuni hiyo iliomba kusisitisha shughuli zake kwa kipindi cha miaka mitano kutokana na bei ya madini hayo kushuka katika soko la dunia na kwamba , suala hilo bado linafanyiwa kazi kitaalam na kiuchumi hivyo, bado serikali haijatoa majibu kuhusu suala husika. 
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) na Mkuu wa MKoa wa Ruvuma Christina Mdeme (kulia ) wakichanganya kokoto katika Kituo ch Umahiri Songea wakati wa ziara Kairuki kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho
Sehemu ya jengo la Kituo cha Umahiri Songea katika hatua zake za ujenzi
Afisa Madini Mkazi wa Songea Abraham Nkya akieleza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Angellah Kairuki alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Waziri wa Madini ANgellah Kairuki akiteta jambo na AFisa Madini Mkazi Mkoa wa Ruvuma Abraham Nkya wakati wa ziara ya Waziri Kairuki kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea. Wa Pili Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mdema , Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Madini Gladness Mkambaita na wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini, Andrew Eriyo. 




Hivyo makala SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI

yaani makala yote SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/serikali-haijaruhusu-uchimbaji-madini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI HAIJARUHUSU UCHIMBAJI MADINI MTO MUHUWESI- KAIRUKI"

Post a Comment