title : RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU
kiungo : RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU
RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa walimu kuendelea kuwa walezi wa wanafunzi wao na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoharibu haiba na heshima ya ualimu, ili waweze kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili kwao na wanafunzi wanaowafundisha.
Mtaka ameyasema hayo Novemba 28, 2018 katika mahafali ya 26 ya kidato cha nne shule ya sekondari Mwembeni (ambayo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 1997-mwaka 2000), iliyopo Mjini Musoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Amesema katika baadhi ya maeneo baadhi ya walimu wamekuwa wakifanya mambo ambayo yanaharibu heshima na haiba ya ualimu jambo ambalo linapelekea wazazi kutowaamini walimu na kuogopa kuwapeleka watoto wao katika shule hizo.
" Naishukuru sana bodi ya shule na walimu wa Mwembeni kwa kuendelea kuhakikisha walimu wetu wanalinda heshima na haiba ya ualimu na wazazi wameendelea kuiamini shule kwa kuleta watoto wao, kwa sababu hakuna matukio yanayohatarisha uwepo wa watoto wao shuleni na masuala la elimu, maadili na nidhamu kwenye shule hii kama Taasisi yameendelea kuimarishwa" alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni Mjini Musoma, ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Mwl.Anselm Mnibhi wa Shule ya Sekondari Mwembeni ambaye pia alimfundisha yeye akiwa mwanafunzi wa shule hiyo mwaka 1997-2000, wakati wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo, iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye kipaza sauti) akiwa na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliwafundisha, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wakurya, katika mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliowafundisha, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU
yaani makala yote RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/rc-mtaka-atoa-wito-kwa-walimu-kuepuka.html
0 Response to "RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU"
Post a Comment