title : DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA.
kiungo : DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA.
DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi', amesema CCM inasimamia Sera zake ipasavyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii na kiuchumi.
Kauli hiyo ameitoa leo katika mwendelezo wa ziara yake kwa siku ya tatu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' Zanzibar.
Amesema CCM inaamini kwamba suala la maendeleo kwa jamii halina itikadi za kisiasa bali linatakiwa kutekelezwa kwa wananchi wote bila ya ubaguzi, hatua ambayo imefikiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa ugatuzi wa madaraka katika Serikali za Mitaa.
Ameeleza kwamba fikra na dhana ya zanzibar kuwa 'Singapore' ya Bara la Afrika inaendelea kutekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na CCM kupitia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Amesema sifa kuu ya viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi ni uadilifu, hekima, busara, ukweli, utu na uongozi bora katika kutatua kero za wananchi.Kupitia ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo, Dk. Mabodi amewaonya baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani nchini kuacha tabia ya kupotosha umma kwa makusudi juu ya hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa na Serikali katika Sekta ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia na kueleza kuwa Sera hiyo ipo katika Ilani ya CCM na inaendelea kutekelezwa kwa kufuata matakwa ya kisheria.
" Kuna baadhi ya watu wanaojiita wanasiasa hapa Zanzibar wao kazi yao kubwa ni kuisubiri Serikali itekeleze jambo lolote la maendeleo, na wao waibuke na kukosoa na kubeza bila ya hoja za msingi ili waweze kupata siku za kuishi kisiasa.
NAIBU katibu Mkuu CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini MAGHARIB Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud wakikagua machine ya wajasiriamali wa kuuza dagaa huko Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A' Unguja.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
Hivyo makala DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA.
yaani makala yote DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dk-mabodi-afanya-ziara-ktk-manispaa-ya.html
0 Response to "DK. MABODI AFANYA ZIARA KTK MANISPAA YA MAGHARIB 'A' UNGUJA."
Post a Comment