Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge
kiungo : Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge

soma pia


Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge


Frank Mvungi- MAELEZO, Njombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kuendelea kuwawezesha wajasiriamali kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) .

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku 10 kwa wajasiriamali zaidi ya 700 wa Mjini Njombe Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Christopher Ole Sendeka amesema kuwa swala la urasimishaji Biashara kwa wajasiriamali ni takwa la Kisheria na pia ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ibara ya 58 ambapo Biashara zote zinatakiwa kuendeshwa katika mfumo rasmi na Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo mkubwa ili kuwainua wajasiriamali wanyonge.

“ Nawapongeza MKURABITA na Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa kufanikisha mafunzo haya kwa wajasiriamali yanayolenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao na pia kuanzishwa kwa Kituo Kimoja cha Urasimishaji Biashara hapa Njombe itakuwa ukombozi kwa wajasiriamali wetu”; Alisisitiza Ole Sendeka.

Akifafanua Mhe. Ole Sendeka amesema kuwa kuanzishwa kwa Kituo cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara Mjini Njombe kumewashirikisha wadau kama MKURABITA, TRA, SIDO na Benki mbalimbali ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kukabiliana na tatizo la Ongezeko la Biashara ndogo na za kati zisizo rasmi na ambazo zinakuwa kwa kasi.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akifunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 700 wa Mjini Njombe yaliyoratibiwa na Ofisi ya Rais, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili waweze kurasimisha Biashara zao. Hayo yamejiri leo tarehe 17/11/2018 Mjini  humo. 
Sehemu ya Wajasiriamali hao zaidi ya 700 wa Mjini Njombe wakifuatilia hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika mjini humo ambapo Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Christopher Ole Sendeka alikuwa mgeni rasmi. Mafunzo hayo  yamelenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili waweze kurasimisha Biashara zao. 
Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akizungumzia faida za mafunzo waliyopata Wajasiriamali zaidi ya 700 wa mjini Njombe yakilenga kuwajengea uwezo ili warasimishe Biashara zao na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi. 
Mmoja wa wajasiriamali walinufaika na mafunzo yakuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao Bw. Lucas Kawongo akifurahia cheti alichotunukiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe wakati akifunga mafunzo kwa  wajasiriamali zaidi ya 700 wa Mjini Njombe. 
Mhasibu wa Mapato kutoka Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. George C. Mwasera akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili warasimishe Biashara zao.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akiwasili ukumbini  kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 700 yaliyoandaliwa na MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili warasimishe biashara zao. 




Hivyo makala Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge

yaani makala yote Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/rais-dkt-john-pombe-magufuli-apongezwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge"

Post a Comment