title : KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA KUKAGUA USALAMA WA VIVUKO MIKOA YA KUSINI
kiungo : KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA KUKAGUA USALAMA WA VIVUKO MIKOA YA KUSINI
KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA KUKAGUA USALAMA WA VIVUKO MIKOA YA KUSINI
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wan nne kulia) akitoa maelekezo kwa mafundi wakati akikagua fitokombo (‘crankshaft’) mashine ya kuchonga vipuri vya injini za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Mtwara wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo.Wa pili kulia ni Kaimu Meneja wa TEMESA mkoa huo Rocky Sabigoro.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akimpa maelekezo Mkuu wa Kivuko Kilambo Namoto ndugu Dhulkif Hamdan kulia wakati wa ziara yake ya kukagua usalama wa vivuko katika mikoa ya kusini. Kivuko cha MV. KILAMBO kinatoa huduma kati ya Kilambo na Namoto mkoani Mtwara.
Abiria wa kivuko cha MV. KITUNDA kinachotoa huduma kati ya Kitunda na Lindi mjini wakimsikiliza kwa umakini mfanyakazi wa kivuko hicho wakati akiwapa elimu ya jinsi ya kuvaa boya la kujiokolea pindi inapotokea ajali ya maji.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akitoa maagizo kwa Meneja wa TEMESA mkoa wa Lindi Mhandisi Grayson Maleko kulia wakati akikagua ujenzi wa jengo la abiria kusubiria kivuko (‘waiting lounge’) katika kivuko cha Lindi kitunda. Majengo hayo pamoja na vyoo yanajengwa pande zote mbili za kivuko na yanatarajiwa kumalizika hivi karibuni na kuanza kutumiwa na abiria wa kivuko hicho.
Abiria wa kivuko cha MV. KITUNDA kinachotoa huduma kati ya Kitunda na Lindi mjini mkoani Lindi wakishuka kutoka kwenye kivuko hicho baada ya kuwasili kutokea Kitunda. Kivuko hicho kimekua msaada mkubwa kwa wakaazi wa maeneo hayo ambao kabla ya ujio wa kivuko walikua wakivuka kwa kutumia mitumbwi midogo ambayo ilikua ikihatarisha usalama wao kwa kiasi kikubwa.
Kivuko cha MV. KITUNDA kikielea majini wakati kikikaribia maegesho ya Lindi Mjini kutokea Kitunda. Kivuko hicho kimekua msaada mkubwa kwa wakaazi wa maeneo hayo ambao kabla ya ujio wa kivuko walikua wakivuka kwa kutumia mitumbwi midogo ambayo ilikua ikihatarisha usalama wao kwa kiasi kikubwa.
Hivyo makala KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA KUKAGUA USALAMA WA VIVUKO MIKOA YA KUSINI
yaani makala yote KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA KUKAGUA USALAMA WA VIVUKO MIKOA YA KUSINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA KUKAGUA USALAMA WA VIVUKO MIKOA YA KUSINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/kaimu-mtendaji-mkuu-temesa-afanya-ziara.html
0 Response to "KAIMU MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA KUKAGUA USALAMA WA VIVUKO MIKOA YA KUSINI"
Post a Comment