title : PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA
kiungo : PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA
PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amefanya ziara katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji kwa lengo la kuhakikisha lengo la Serikali kuwapatia wananchi huduma ya majisafi na salama linatimia.
Akiwa wilayani humo Profesa Mbarawa amejionea changamoto mbalimbali zinazosababisha utekelezaji usioridhisha na kuwataka watendaji wa wilaya hiyo kuchukua hatua sahihi ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika, ambapo baadhi yake imeanza mwaka huu na mingine ni ya muda mrefu.
Profesa Mbarawa ametembelea miradi ya Kakonko Mjini, Muhange, Kiga, Gwanumpu na Nagwijima kwa lengo la kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa miradi hiyo. Akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Kakonko, Profesa Mbarawa amewataka watendaji hao kuhakikisha wanachukua hatua, ikiwemo kuvunja mikataba ya wakandarasi wanaoonekana kukosa uwezo wa kutekeleza miradi hiyo kwa kufuata taratibu za kisheria na kutafuta wakandarasi wanaoweza kufanya kazi nzuri.
Profesa Mbarawa amesema anataka kuona miradi yote wilayani Kakonko inakamilika kwa wakati ikiwa ni sehemu ya kutekeleza lengo la Serikali kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi kwa kuwa fedha za kutimiza lengo hilo zipo, hivyo haoni sababu ya kutokukamilika kwa miradi ya maji.
Huku akitaka kuwe na mawasiliano mazuri kila baada ya miezi miwili kati ya watendaji, wabunge na viongozi wa Serikali kuhusu maendeleo ya miradi kwa kila hatua ya utekelezaji. Wakati huo, Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza amesema utendaji wa wataalamu umekuwa kikwazo kikubwa kwa Serikali, kutokana na kutokufuatwa kwa taratibu sahihi za manunuzi na usimamizi mbovu wa miradi ya maji.
Mhandisi Chiza amewaasa watendaji wa Serikali wenye dhamana ya usimamizi wa miradi ya maji kutumia taaluma zao vizuri ili kupata matokeo chanya kwenye miradi ya maji.

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mhandisi wa Wilaya ya Kakonko (kushoto), Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza (kulia) pamoja na na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala kwenye Mradi wa Maji wa Gwanumpu katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma. 
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji cha Muhange wakati alipofanya ziara kwa lengo la kujua hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia) akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza wakiwa pamoja na na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala kwenye Mradi wa Maji wa Nyagwijima katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.
Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza akimuongoza Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa wakitoka kwenye Chanzo cha Maji cha Mugembezi kinachotumika kwa ajili ya Mradi wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko, mkoani Kigoma.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na akina mama kijijini Kiga mara baada ya kujionea mradi wa Kiga na kuzungumza na Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Mradi wa Maji wa Kiga katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.

Hivyo makala PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA
yaani makala yote PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/profesa-mbarawa-yuko-wilayani-kakonko.html
0 Response to "PROFESA MBARAWA YUKO WILAYANI KAKONKO KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA"
Post a Comment