title : Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya
kiungo : Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya
Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya
Wataalam wa afya wameshauriwa kuendelea kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru wakati akifunga kongamano la pili la kisayansi la Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Prof. Museru ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kufanya tatifi kwani zitawezesha hospitali kutibu wagonjwa kutokana na rasimali zilizopo na kwamba tafiti pekee ndio itafanikisha wataalam kuendelea kutoa huduma bora zaidi.
Amefafanua kuwa tafiti zinasaidia kutatua matatizo yaliyopo sehemu za kazi hivyo ameahidi kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili itaendelea kuwawezesha watalaam wake katika kufanya tafiti ambazo zitaleta tija katika utoaji wa huduma.
Pia, Profesa Museru ametumia fursa hiyo kuwatunuku vyeti pamoja na fedha Madaktari Bingwa wawili wa Muhimbili ambao wamefanya tafiti ambazo zitaleta mabadiliko katika kuhudumia wagonjwa.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura, Dkt. Juma Mfinanga amefanya utafiti wa kuangalia ubora wa magari ya kubebea wagonjwa pamoja na changamoto zake.
Utafiti huo utasaidia kubaini tatizo lililopo katika kusafirisha wagonjwa kuanzia eneo la tukio mpaka hospitalini pamoja na huduma za dharura zinazotolewa kabla ya mgonjwa kufika hospitalini.
Vilevile utafiti huo utawezesha kutoa muongozo jinsi ya kuhudumia wagonjwa wa dharura kuanzia eneo la tukio mpaka hospitalini na kupunguza vifo vinavyotokea nje ya hospitali.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani, ubongo na mishipa ya fahamu, Dkt. Kigocha Okeng’o, yeye amefanya utafiti ulioangalia viashiria vya kupona haraka kwa mtu aliyepata ugonjwa wa kiharusi.
Katika kongamano hilo la siku mbili, mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo tiba kwa mama ambaye anatoka damu nyingi baada ya mimba kuharibika, mama kushindwa kuzuia haja ndogo baada ya kufanyiwa upasuaji, matumizi ya rekodi za wagonjwa kwa ajili ya tafiti, upanuzi wa huduma za magonjwa ya dharura nchini, afya ya akili na magonjwa ya kisukari.
Zaidi ya wataalam wa afya 200 wameshiriki katika kongamano hilo ambalo limebaba kauli mbiu inayosema “utoaji wa huduma bora za afya Tanzania hususani huduma ya afya ya mama na uzazi.’’
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza katika kongamano la pili la kisayansi kuhusu wataalam wa afya kutoa huduma bora kwa mama na mtoto. Prof. Museru amefunga kongamano hilo leo ambalo lilianza jana.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Prof. Museru kwenye kongamano hilo.
Prof. Museru akimtunuku cheti Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga baada ya kufanya utafiti kuhusu ubora wa magari ya kubeba wagonjwa lengo likiwa ni kuboresha huduma hiyo nchini. Katikati ni Kaimu Mkurungenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Zuhura Mawona.
Kutoka kushoto ni Dkt. Juma Mfinanga ambaye ameandika utafiti kuhusu ubora wa magari ya kubeba wagonjwa, Mkuu wa Kitengo cha Utafiti Muhimbili, Dkt. Faraja Chiwanga na kulia ni Dkt. Kigocha Okeng’o wa Muhimbili ambaye amefanya utafiti ulioangalia viashiria vya kupona haraka kwa mtu aliyepata ugonjwa kiharusi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada na waandaji wa kongamano hilo.
Hivyo makala Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya
yaani makala yote Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/muhimbili-yasisitiza-wataalam-kufanya.html
0 Response to "Muhimbili yasisitiza wataalam kufanya tafiti za afya"
Post a Comment