MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI

MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI
kiungo : MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI

soma pia


MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI


Siku ya Jumanne, tarehe 24 Septemba 2018, Mtanzania Gerald Bigurube alitunukiwa tuzo ya mwaka 2018 ya Ujerumani na Afrika (2018 German Africa Award). Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwake na Dr. Wolfgang Schäuble, Rais wa Bunge la Ujerumani Bundestag. Mwaka huu tuzo hiyo ilitolewa kwa watu wawili, mwingine akiwa ni Bw.

Bw. Gerald Bigurube ametumia kipindi cha miaka arobaini na nne katika Maisha yake kutunza wanyama pori na mazingira. Alipokuwa kiongozi wa TANAPA, Bw. Bigurube (miaka 66), alipambana dhidi ya ujangili, na alifanya juhudi za kuleta uwiano sawa baina ya utunzaji misitu na Wanyama pori kwa upande mmoja, na maisha ya wanadamu na maendeleo ya kiuchumi kw aupande mwingine. Bw. Bigurube ametoa mchango mkubwa kuonyesha jinsi utunzaji wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi vinavyotegemeana.

Kwa sasa, Bw. Bigurube anafanya kazi kama mkurugenzi mkaazi wa Frankfurt Zoolocal Society, taasisi ya kimataifa inayojihusisha na utunzaji wa mazingira, yenye makao yake mjini Frankfurt Ujerumani. Taasisi hiyo inafanya kazi kwa karibu na mamlaka za hifadhi nchini Tanzania, hususan katika kupambana na ujangili.

Ushirikiano wa mamlaka za Serikali ya Tanzania na Frankfurt Zoolocal Society umeiwezesha Tanzania kupata mafanikia katika utunzaji wa mazingira na kukabiliana na ujangili. Mpaka sasa, Tanzania imeweza kutenga maeneo takriban asilimia 32 ya ardhi yote kama hifadhi za taifa, na kuifanya kuwa ndiyo nchi yenye eneo kubwa zaidi la hifadhi barani Afrika.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Possi, amempongeza Bw. Bigurube kwa moyo wa uzalendo aliokua nao. Dkt. Possi pia amewahimiza wadau wa mazingira kuzidi kufanya kazi kwa karibu na Tanzania, haswa ukizingatia kwamba kazi ya Utunzaji wa mazingira inayofanywa na Tanzania pia ina manufaa kwa ulimwengu mzima.

Dkt. Possi alifafanua, juhudi za kutunza mazingira Tanzania zitafanikiwa zaidi iwapo kutakuwa kuna ushirikiano utakaoiwezesha Tanzania kupata teknolojia bora itakayorahisisha matumizi bora ya ardhi katika shughuli za binadamu, na kwa maana hiyo, nchi zilizoendelea na Taasisi mbalimbali za kimataifa zinapaswa kuzingatia kwamba masuala kama vile kilimo cha kisasa na upatikanaji wa uhakika wa nishati ni muhimu katika utunzaji wa mazingira.


Hivyo makala MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI

yaani makala yote MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mtanzania-gerald-bigurube-atunukiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MTANZANIA GERALD BIGURUBE ATUNUKIWA TUZO UJERUMANI"

Post a Comment