Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili

Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili
kiungo : Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili

soma pia


Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vifaa tiba aina ya Stents vyenye thamani ya Tshs. 86.2 milioni kutoka kampuni ya Boston Scientific ya Marekani kwa ajili ya wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula. 

Stents ni vifaa maalum mithili ya springi ambavyo vinaweza kuwa vya plastiki au chuma vyenye uwazi katikati wanavyowekewa wagonjwa wenye uvimbe kwenye koo lililoziba ili kupanua sehemu hiyo na kuruhusu kupitisha chakula. Kuna stents za aina mbalimbali kutegemeana na mgonjwa ana shida ya aina gani. 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, Dkt. Masolwa Ng’wanasayi amesema kampuni hiyo imetoa stents 25 ambazo zitatumika kwa wagonjwa 25 wenye satarani ya koo la chakula ili kuwasaidia kumeza chakula na kuendelea na matibabu ya mionzi. 

“Mgonjwa mwenye tatizo la saratani ya koo la chakula, anakuwa hawezi kumeza chakula na hali hii inasababisha mgonjwa kupungua uzito na kushindwa kuendelea na matibabu mengine, hivyo vifaa hivi vitawasaidia kumeza chakula na kuendelea na matibabu mengine,” amesema Dkt. Ng’wanasayi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hopitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akipokea kifaa tiba cha aina ya STENTS kwa ajili ya wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Boston Scientific ya Marekani, Troy Lengel. Wengine kushoto ni wawakilishi kutoka hospitali ya Muhimbili, Mayo Clinic ya Marekani na Chuo Kikuu cha San Francisco nchini Marekani na kulia ni wawakilishi kutoka MUHAS na Hospitali ya Muhimbili.
Pichani ni vifaa tiba aina ya STENTS ambavyo wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula wameanza kuwekewa ili kuwasaidia kumeza chakula kutokana na mfumo wa koo kuharibiwa na ugonjwa huo. 



Hivyo makala Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili

yaani makala yote Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/msaada-wa-tshs-86-mil-kunufaisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili"

Post a Comment