title : MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO APOKEA MADAWATI 50 KUTOKA BENKI YA NMB
kiungo : MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO APOKEA MADAWATI 50 KUTOKA BENKI YA NMB
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO APOKEA MADAWATI 50 KUTOKA BENKI YA NMB
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi. Beatrice Dominic leo amepokea madawati 50 yaliyotolewa na benki ya NMB katika shule ya Msingi Ubungo Plaza
*"Kwa namna ya pekee nichukue fursa hii kuishukuru NMB kwa kuona uhitaji wetu na kuamua kutusaidia madawati haya".* Alisema bi. Beatrice.
Mkurugenzi alisema kwamba atahakikisha mahusiano kati ya benki na Halmashauri yanadumishwa na NMB wasiishie tu kwenye madawati kwani wananchi wa Manispaa ya Ubungo bado wana mahitaji mengi.
Vile vile Mkurugenzi aliuomba uongozi wa benki kufikiria juu ya ujenzi wa uzio kwa upande wa mbele ya shule hiyo .
Aidha aliwaasa watoto kusoma kwa bidii na kuyatunza vizuri madawati hayo ili hata wadogo zao wapate nafasi ya kuyatumia.
Nae Meneja Uhusiano wa benki ya NMB bi. Vicky Vishubo alisema uongozi wa NMB hautoishia tuu kwenye madawati kwani wana mpango wa kuendelea kutoa misaada Halmashauri ya Ubungo kwa maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
Aliongeza kuwa benki ya NMB itaendelea kutoa ushirikiano katika maeneo tofauti toafauti kama kwenye elimu, afya na upande wa michezo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule bw. Ramadham Maughuu aliwashukuru benki ya NMB na Uongozi wa Manispaa kwa msaada walioupata.
Lakini pia aliwaomba kuiangalia shule ya Ubungo Plaza kwa jicho la tatu katika suala la kuwajengea uzio wa mbele ya shule na ofisi za walimu.
*IMETOLEWA NA*
*OFISI YA HABARI NA UHUSIANO*
*MANISPAA YA UBUNGO*
Hivyo makala MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO APOKEA MADAWATI 50 KUTOKA BENKI YA NMB
yaani makala yote MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO APOKEA MADAWATI 50 KUTOKA BENKI YA NMB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO APOKEA MADAWATI 50 KUTOKA BENKI YA NMB mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mkurugenzi-wa-manispaa-ya-ubungo-apokea.html
0 Response to "MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO APOKEA MADAWATI 50 KUTOKA BENKI YA NMB"
Post a Comment