title : MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI
kiungo : MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI
MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuagiza upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa serikali kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kulifuatilia jalada la kesi hiyo na Novemba 17, 2018 waje kueleza maendeleo halisi ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameeleza hayo leo Novemba 5, 2018 Kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa. Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kuieleza Mahakama kuwa Kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika na kwamba DPP ametoa maelekezo ambazo yanafanyiwa Kazi.
Baada ya maelekezo hayo, wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko ameeleza kuwa, inaumiza sana, ni mwaka sasa umepita shtaka moja lakini upelelezi wake bado haujakamilika huku dhamana ya washtakiwa ikiwa imezuiwa na kuhoji kuna makesi yenye mashtaka mengi upelelezi wake umekamilika ndani ya miezi mitatu, hili shtaka moja linatimiza mwaka mmoja unaenda wa pili sasa.
Amedai, shtaka linalowakabili washtakiwa hao, limejitosheleza na lina kila kitu toka mwaka Jana lugha ni hiyo hiyo upelelezi haujakamilika.
Mheshimiwa, tunaamini kiwa DPP anapozuia dhamana ya mtu basis huyo mtu atasikilizwa kwa wakati, tunaomba Mahakama iwalazimishe upande Wa mashtaka watueleze msimamo halisi wa upelelezi ili tujue wamekwama wapi na sisi tufuatilie." Alieleza Nkoko.
Baada ya kusikiliza hoja zote, Hakimu Mashauri emeutaka upande wa mashtaka kulifuatilia jalada hilo la kesi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 17. Mwaka huu.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort) Archard Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini,
Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kutokana na DPP kuzuia dhamana zao na Wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya sh 2.4 bilioni.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabilkiwa na ashtaka la kuisababishia serikali hasara ya sh 2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.
Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 ambazo ni sawa na sh 2,486,397,9.
Hivyo makala MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI
yaani makala yote MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mahakama-yauagiza-upande-wa-mashtaka_5.html
0 Response to "MAHAKAMA YAUAGIZA UPANDE WA MASHTAKA KUFUATILIA JALADA KWA DPP, KESI YA VIGOGO WAWILI WA UTHAMINI WA MADINI YA ALMASI"
Post a Comment